Msaada wa tathimini kwa hii ramani

Unaweza kuwa sahihi.
Ila kuna watu wanamitazamo tofauti, mfano, kuna anayependelea chumba cha watoto wa kike kikae mbali na wakiume, ataweka wapi kwa kipato chake kinachoruhusu nyumba ya ukubwa huo halafu master pia aiweke mbali.
Umesema kuongeza kila chumba na choo chake, ukubwa huo wateja wengine hawawezi hasa wale waliotoka kupanga chumba na sebule, wakajibana wakaweza kujenga house ya ramani hiyo.
Kupita nyikoni ukienda uani hilo sio tatizo kwa watu wengi mana jiko sio chumba cha kulala.
Mzunguko wa hewa sebuleni, unaweza kuwa mzuri yakiwekwa madirisha makubwa na uelekeo kutegemea site ilivyo. Sebule kumbuka ni mpaka dinning ndio mana pale pakatenganishwa na uwazi ambao unachukua hewa kupitia madirisha ya dinning.
Kila mtu ana vionjo vyake, kibaya kwako chaweza kuwa kizuri kwake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…