Msaada wa tatizo la Kelele kwenye engine ninapowasha gari

Msaada wa tatizo la Kelele kwenye engine ninapowasha gari

shalet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2013
Posts
3,430
Reaction score
3,547
Habari wataalamu kwa wiki kama mbili nimenotisi kitu kwenye gari yangu. Nikiwasha asubuhi. Inakuwa na kamlio fulani kwenye engine ambapo kanapotea baada ya dakika kama mbili au tatu gari ikipata moto.

Nilipelka jana kwa fundi akanishauri nibadilishe oil pengine ipo chache. Leo tena nimeona shida ileile.
Nimerekodi sauti yake kwa anayeweza toa suggestions.

Nipo kigamboni gari ni subaru forester.
 
Kelele zenyewe ni kama mtu anapuliza filimbi
 
Kuna vitu vingi vinavyoweza sababisha gari kutoa mlio,vitu kama berings za Ac au oil pump inaweza sababisha mvumo,...oil pia kutopanda vizuri kuna sababisha vyuma kupiga ka ukelele flani....mimi kwakua najua mafundi wengi wa Dar ni wazee wa kukisia kama wapiga ramli....nachofanyaga natafuta namba za simu za mafundi engine wazoefu kama wanne wa gereji tofauti tofauti kupitia njia mbalimbali hasa ma group yangu ya wasap yanayohusu magari,....baada ya hapo naenda na gari nawambia wasikilize mlio huo au kama wewe si unasema imerekodi.....baada ya hapo lazima tapata jibu,baada ya hapo ndio nampa kazi mmoja afanye!
 
Kwa uzoefu hiyo ni belt mkuu inakuaga hivo kwa muda alafu inaisha sababu ya weather(moja ya sababu) ila ikipersist zaidi ya wiki inafaa ubadili belt utakua umemaliza tatizo, inaitwa serpentine belt kitaalam.
 
Back
Top Bottom