Msaada wa tofauti ya hati ya kiwanja na nyumba

T-bane

Member
Joined
Apr 17, 2017
Posts
79
Reaction score
159
Wanasheria heshima kwenu,

kwa uelewa wangu mdogo ni kuwa hati ya kiwanja inapatikana baada ya kupata offer ya kiwanja then ndio baadae unapata hati ya kiwanja (kama nimekosea nisahihisheni kwa hilo).

Sasa endapo mtu umepata offer ya kumiliki kiwanja cha ekari moja; na baadae let say ukajenga nyumba kama vile appartments style zikawa nyumba let say 5 ndani ya kiwanja kimoja cha ekari moja.

Swali: Hati ya nyumba unaipata kutoka wapi? au ile Offer au hati ya kiwanja ndio inakuwa hiyo hiyo hati ya nyumba??

Je endapo nataka kila nyumba niliyojenga iwe na hati yake, nafanyaje?

Naomba ushauri wenu wa kisheria na utalamu wenu kadiri mnavyofahamu.

Natanguliza shukrani.
 
hati ya kiwanja ina PLOT no na hati ya nyumba ina BLOCK no so vyote hivi hupewa kwa wakat mmoja
 
ila hapo kwenye ekar moja ndugu unapata hati moja tu tena yenye maelezo kuwa eneo ni la nini km umeamua ni biashara ya guest shule n.k basi utapewa ramani kamili

lkn hakuna kitu kinachoitwa hati ya kiwanja kimoja chenye hati ya nyumba kumi au ishirini
 
Asante kwa ufafanuzi lakini kidogo umenichanganya. Mfano offer yangu imeandikwa Block M. na kisha kiwanja no.----. Ila hiyo ni offer ambayo inaonyesha umiliki wa kiwanja kwa miaka 33. na wewe umusema offer ina PLOT No. Na pia hati ina BLOCK No. sasa hapo ndio umeniacha njia panda, kwa sababu najua inabidi nifuatilie HATI YA KIWANJA, au nimekosea?
 
Kuna hati ya kiwanja, hakuna hati ya nyumba.
Mwenye kiwanja ndio mwenye nyumba.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa ikiwa mimi nina hiyo hati ya kiwanja na nimejenga nyumba mbili na sasa nataka nimkabidhi nyumba moja mchepuko wangu kwa jina lake, je nafanyaje?

msaada wako tafadhali
 
Kiwanja kikipimwa hupata namba na kitalu ( Plot na block) unapoandaliwa /hati huonyesha namba ya Kiwanja na kitalu.Nyumba hujengwa juu ya hicho Kiwanja hivyo .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ndio fatiia hati ya kiwanja ndo muhimu hiyo ndo itaonesha hadi BLOCK no yako na jinsi ya ujengaji wa nyumba yako inapaswa itizame wapi na geti linakaa wapi kubwa kwa dogo ukishapewa ramani ndio utajenga kanafasi kakibaki hata vyumba vya wapangaji ukijenga ruksa ila hakuna hati ya nyumbs hapo kwenye vyumba vya wapangaji
 
Kuna hati ya kiwanja mkuu hakuna hati ya nyumba...
 
Kwa viwanja vya zamani kabla ya 2008 ilikuwa ukinunua kiwanja unapewa Letter of Offer kutoka Manspaa/Jiji/Halmashauri ya Wilaya ambapo unaweza ukajenga nyumba bila shida ila unatakiwa ufuatilie Hati ya Kiwanja kwa kamishina wa Ardhi ambapo kwa Dar unaenda Wizara ya Ardhi na mikoani kuna ofisi za Kanda. In short Letter of Offer ni document ya temporary ambapo kama hujakiendeleza ni rahisi kuporwa kiwanja chako na kupewa mwingine tofauti na hati. Kikubwa ukiwa na Offer jitahidi ufuatilie hati.

Kuhusu kujenga ukiwa na offer rukhsa kujenga huku unafuatilia hati yako ya kiwanja ambayo lazima upewe kwa kuwa kiwanja kipo surveyed na ndio maana kikapewa Letter of Offer. Kwa sasa Letter of Offer zimefutwa na ukinunua kiwanja ndani siku chache unapewa Hati yako ya kiwanja

Hivyo mleta uzi unatakiwa kujenga kulingana na kiwanja kimetolewa kwa shughuli gani yaani kama nyumba ni ya makazi ama biashara au taasisi ila kikubwa unatakiwa uwe na Building Permit ambayo hayo majengo yote yanakuwa yameonyeshwa kwenye site plan ...yaani kunakuwa na Main House na hizo zingine zinachukuliwa kama nyumba za ziada ..kwa viwanja vya kawaida unaruhusiwa apartment moja ama mbili kulingana na size ya kiwanja ila kwa ekari moja hapo ni kikubwa sana (nakushauri peleka michoro ya nyumba zako Manispaa kwa ajili ya building permit au ukigawe )
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…