Msaada wa ufafanuzi katika ujenzi wa ghorofa moja

Nimepiga hesabu hapa kuwa kwa mwezi ni fight atleast nipate 1.5m ya uhakika itahitaji miaka 7 yaani miezi 84 kufikisha 126m ambayo ndio kighorofa kitaonekana. Duh..
Kama unataka kufanya kitu kianze tu, wala usiwaze hizo hesabu za pesa. Kawaida Mungu anakupa kutakana na mpango ulionao. Ukiwaza kidogo utatumia nguvu ndogo na ukiwaza kikubwa Mungu atakupa nguvu kubwa ukimalize

Mie nimejenga ghorofa ina vyumba vinne, baths tano na sebule chini na juu. Nimejenga kwa miaka mitano mpaka namaliza kila kitu mpk fensi, landscaping na geti.

Nilipoona nimeweza ndio nikaanza kujenga nyumba ndogo simple za kupangisha
 
Hongera sana Kiongozi
 
Ila natamani sana waTanzania tungejifunza kutegemea watalaam kwenye shughuli zetu. Unakuta mtu anajenga nyumba ya bajeti milion 100, lakini ukimwambia amshirikishe architect au engineer hataki.

Cheap is expensive!
Kwa kweli point yako ni muhimu sana kwa watu wanaotaka kujenga (hasa ghorofa) kuizingatia. Ghorofa msingi wake tu unakula zaidi ya milioni 40. Hawa Fundi Maiko atakwambia andaa milioni 15 - 20, matokeo yake nyumba baada ya mwaka mmoja inakuwa na nyufa kibao na baadaye kuanguka kabisa. Mimi binafsi najenga ghorofa, nimeanza mwezi wa 12 mwaka jana. Katika ujenzi huo nilimtafuta Architect mwenye uzoefu akanichorea ramani, akaipeleka kwa Structural Engineer naye akaandaa michoro yake. Baada ya hapo nikamtafuta Engineer mwenye uzoefu mkubwa (nilipewa connection) wa kunisimamia kwenye ujenzi, tukakubaliana gharama za usimamizi. Hadi ninavyoandika muda huu jengo linajengwa mpaka nafurahi, mimi ni kwenda kuangalia tu hatua za ujenzi zilizofikiwa. Huyu Engineer wakati mwingine ananiita site kunipa option ya masuala mbalimbali kulingana na mchoro wa Jengo. Hadi muda huu tupo tunamwaga zege kwenye slab ya ghorofa ya kwanza. Jengo linavutia hata kabla ya kumalizika. Zaidi ya hapo hawafanyi ujenzi wowote bila kufanya material testing.
 
Hongera sana mkuu. Project yako unaiendesha kisomi sana. Hiyo haizuii watu kujenga kawaida, okoa gharama pale penye ulazima.
 
Hizo milioni 40 za msingi wajenga nyumba ya sq ngapi?
Je wajenga na underground?
 
Hii experience sitaki ata kukumbuka. Unzaika nondo na tofali zaidi ya 3000 chini, ila inategemea na ukubwa wa nyumba. Ila ikiisha unaheshimika
 
Daaah hii sio nyumba nikibanda,
Kinafaa ukijenge kwaajili ya kukipangisha
Uapte ata 250k per month
 
Iv mtapigwa mpaka lini icho kibanda ndoo 100m kweli?
 

Eti nimlipe mtu anisaidie kuniimbia![emoji276]tutabanana hapo hapo kisu cha tumbo mguu wa roho,maghorofa yameanza kujengwa kabla hata mnawaita wataalamu hawajazaliwa
 
Uko vizuri kaka umetoa maelezo mazuri sana kwa aliye makini atakuelewa. Pia umenisaidia sana maana soon nina project ya kujenga nyumba ya ghorofa moja. Hii itanisaidia kukadiria materials na gharama za uendeshaji wa kazi pia.
 
thanks for sharing.
 
thanks for sharing.

Kaka umeelezea vizuri sana ahsante kwa moyo wako hakika Mwenye nia ya kweli amejifunza kitu naomba ushauri wako mim nimejenga nikanunua vyoo vile vya kuchimbia Matank ukutani sasa fundi hakunishauri vizuri nikamwaga na zege sehemu niliyoweka matank sasa Kuna tank moja choo chake ni European( cha kukaa) lakin mim nikamodify nikaweka kwenye Asian toilet (choo cha kuchuchumaa) bomba lake la maji ni nchi mbili sasa ukiflush maji yanatoka kidogo na bila pressure issue inaweza kuwa ni nin na hiyo sehemu mpka tiles nimeshaweka inaniuma kweli kuvunja tena .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…