Msaada wa ujauzito

Chokochoko

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2011
Posts
438
Reaction score
184
Jf natumaini tumeupokea mwaka vizuri na kwa upande wangu naona nimeupokea mwaka vizuri zaidi maana nina ujauzito unaelekea miezi mitatu sasa bado sijaanza kliniki tatizo langu ni hili hapa naombeni ushauri wenu kwa yeyote anaejua huwa napata kiu kali ya maji mara kwa mara nanakunywa maji ila kiu haiishi pia nakojoa mara kwa mara pia nimepoteza hamu ya kufanya tendo la ndoa kabisa nasijisikii kukutana na mpenzi wangu kabisa nimekuwa mkavu na sisimki kabisa je hili ni tatizo la kiafya? sina hali mbaya ya kichefuchefu, kutapika wala kutema mate ovyo ikitokea ni kwa mbali halafu inapotea tofauti na wajawazito wengine japo baadhi harufu sipatani nazo.

je huku kunywa maji kila mara ni tatizo gani?

kutokupata kichefuchefu wala kutapika nitatizo?


tatu nisipofanya tendo la ndoa hadi nizaea kuna tatizo wakati wa kijifungua?


Ni hayo tuu wapendwa naombeni msaada kwa yeyote anaeelewa haya maswala.
 
kapime kisukari kwani baadhi ya dalili ulizosema zina uhusiano na kisukari Zingatia! Sisemi una kisukari la
 
Hiyo heading imenifanya nije kwa kasi, kumbe tayari mjamzito. Ni vema kwa masuala nyeti kama hayo ukamuona mtaalam ili uwe na amani moyoni. Huyo atakupima na kukupa ushauri.
 

Kamuone Mtaalamu wa Afya akusaidie, kwa sababu pale watachukua vipimo mbalimbali na utajua unasumbuliwa na nn
 
hongera mama kijacho! sina experianve kubwa lakn nnachoamini,ni hali ya mapito ya ujauzito itakwisha !
 
Kwanza nikupongeze kwa kupata mimba,wakati wa ujauzito kunamabadiliko mengi ya hormone yanayosababisha damu kuongezeka,kumbuka sehemu kubwa ya damu ni maji.Matokeo yake ni kuwa na maji mengi ya ziada(extra fluid) yanayokuwa processed kwenye figo na kwenda kwenye kibofu cha mkojo.

Unajisikia kukojoa mara kwa mara kutokana na pressure kwenye kibofu kutokana na uterus inayobeba mtoto kuendelea kukua na kuibada bladder,hivyo hata kama bladder haijajaa unajisikia kukojoa.

Kuhusu kunywa maji unakunywa kwa sababu unapoteza maji mengi kupitia mkojo ni lazima kurudisha yanayopotea ni kawaida.

Kichefuchefu si lazima kila mmjamzito apate kichefuchefu inategemea na hormone zake pia jinsi zinavyobadilika.

kukosa hamu ya kumega mkate(tendo la ndoa) yawezakuwa nimabadiliko ya hormone jitahidi kuvuta hisia na may be dear wako aanze kukuandaa mapema kabla ya kushiriki meza takatifu.

Faidi ya tendo ni kuwa inaifanya njia(uke)kuwa laini inakuwa rahisi kutanuka wakati wa kujifungua mtoto anapotoka,usipofanya inakuwa rigid sana inatanuka kwa shida,pia nafikiri utamtesa dear wako loh!
 
Naomba kujua, umeolewa? Hio mimba uliikusudia au ilikua ajali kazini? Then mengine yatafuata.......!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…