Chokochoko
JF-Expert Member
- Oct 15, 2011
- 438
- 184
Jf natumaini tumeupokea mwaka vizuri na kwa upande wangu naona nimeupokea mwaka vizuri zaidi maana nina ujauzito unaelekea miezi mitatu sasa bado sijaanza kliniki tatizo langu ni hili hapa naombeni ushauri wenu kwa yeyote anaejua huwa napata kiu kali ya maji mara kwa mara nanakunywa maji ila kiu haiishi pia nakojoa mara kwa mara pia nimepoteza hamu ya kufanya tendo la ndoa kabisa nasijisikii kukutana na mpenzi wangu kabisa nimekuwa mkavu na sisimki kabisa je hili ni tatizo la kiafya? sina hali mbaya ya kichefuchefu, kutapika wala kutema mate ovyo ikitokea ni kwa mbali halafu inapotea tofauti na wajawazito wengine japo baadhi harufu sipatani nazo.
je huku kunywa maji kila mara ni tatizo gani?
kutokupata kichefuchefu wala kutapika nitatizo?
tatu nisipofanya tendo la ndoa hadi nizaea kuna tatizo wakati wa kijifungua?
Ni hayo tuu wapendwa naombeni msaada kwa yeyote anaeelewa haya maswala.