Msaada wa ushauri GREAT THINKERS

Msaada wa ushauri GREAT THINKERS

SukariTamu

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2013
Posts
295
Reaction score
59
Habari wakuu...poleni na majukumu ya kulijenga taifa letu changa...Wakuu nilimaliza kidato cha nne mwaka 2007 na nilipata daraja la pili la alama 21..kutokana ufukara nilishindwa kuendelea na masomo japo nilichaguliwa kuendelea na masomo ...mwaka huu nimeamua kuendelea na Elimu, je wakuu kwa matokeo yangu ninaweza kupata nafasi katika Chuo cha Ualimu au Fani ingine ukizingatia nimekaa mtaani muda mrefu..N:B Naomba ushauri na sio kejeli
 
Mkuu maswala ya ualim weka pemben...nenda hata diploma ya engineerin..biashara...science..ualim hutatoka tz ya sasa...chek na uezekano wa form five...
 
Ualimu ni kujitakia umaskini tu mkuu.somea ishu za maana kama uhasibu,uhandisi nk.
 
Habari wakuu...poleni na majukumu ya kulijenga taifa letu changa...Wakuu nilimaliza kidato cha nne mwaka 2007 na nilipata daraja la pili la alama 21..kutokana ufukara nilishindwa kuendelea na masomo japo nilichaguliwa kuendelea na masomo ...mwaka huu nimeamua kuendelea na Elimu, je wakuu kwa matokeo yangu ninaweza kupata nafasi katika Chuo cha Ualimu au Fani ingine ukizingatia nimekaa mtaani muda mrefu..N:B Naomba ushauri na sio kejeli

niweke alama ya matokeo yako kwa kila somo kama hutojali tunaweza shauriana na wewe ukafikia malengo fulani...
 
Ualimu ni kujitakia umaskini tu mkuu.somea ishu za maana kama uhasibu,uhandisi nk.

kila mtu akifuata ushauri wako kua asisomee ualim,je watoto wako watasomeshwa na nani???
 
Back
Top Bottom