Msaada wa ushauri/Nasaha..

Pole kwa uliyopitia,lakini mshukuru Mungu wako kwani atakuwa amekuepushia balaa kubwa zaidi. Anza kujipanga upya na utafanikiwa tu.

This one also rises me up..kwamba yamkini nimeepushwa balaa zaidi. Look, gari ya abiria (coaster) nilogongana nayo walikufa watu sita at par (sad)....ati mimi nikabaki hai na kigari changu kidogo..great miracle...God have mercy on me..
 
mkuu pole sana na yaliyokupata amini ndio mitihani ya maisha , ila elewa hakuna mapenzi ya mbali .... cha msingi mshukuru mungu kwa kukuepusha na ajali hiyo na kaa chini utulize mawazo jipange kivyako kimaisha haya mambo ya mali ni ya kupita wewe ni mwanaume ni mpiganaji jipange upya na kama umeandikiwa moja utapata kama ni mbili utapata
 

Asante mkuu.. ila hapo kusema hakuna mapenzi ya mbali.?????? Labda ni tafsiri ya kizazi chetu hiki kilichojaa uchakachuliwaji.. anyways, namshukuru Mungu kwa yote..
 
Ndugu Mtoa Mada.
Mawazo yote uliyopewa humu ni ya maana sana.
Mshukuru Mungu, huyo dada kaonesha tabia hizo kabla hamjaoana. Mabadiliko uliyoyaona ilikuwa ni Mpango wa Mungu wa kukuokoa ili usikumbane na dhahama ya badiliko la tabia wakati mkiwa tayari kwenye ndoa. Hilo lingekuumiza sana, na labda kupata mental breakdown. Una bahati sana Ndugu yangu. Shukuru kila siku kwa hilo kwani ni bora kumshtukia mchumba asiye Mwaminifu kuliko Mke wa ndoa asiye Mwaminifu. Zingatia (kama wewe ni Mkristo) ndoa haivunjwi kirahisi.
Jambo jingine; wewe ni kijana unayeonekana kuwa mwenye Elimu nzuri na umri wa kadiri. Ukijaaliwa kupata kazi, ni kipindi kifupi sana utarejesha unavyohisi umepoteza.
Jitahidi kutokuwa Mwenyewe. Kaa kwny vikundi. Badilishana mawazo na watu mbalimbali. Kamwe usikae mwenyewe, ni hatari. Jihadhari SANA na ulevi wa aina yoyote. Sikushauri ujiingize kwny mahusiano mapya ya kimapenzi. Kuna hatari ukaangukia pabaya. Subiri kidogo.
Natamani ningekuona lkn
Zingatia hayo kwanza.
 
Pole sana Mkuu, huyo haupo tena moyoni mwake utakonda bure kwa mawazo, tafuta atayekufaa.
 

Sawa mkuu nimekupata..labda ningetumia hekima yasingenipata yote hayo ..kuhusu kudai gari,, nikuwa alinioneshea dharau na kibri., akisahau Hali ya maisha nilomkuta nayo..nikaona nivema anunuliwe zuri zaidi na huyo bwanamkubwa ..anyways ..my fault ..and. life goes on.
 
Asante mkuu.. ila hapo kusema hakuna mapenzi ya mbali.?????? Labda ni tafsiri ya kizazi chetu hiki kilichojaa uchakachuliwaji.. anyways, namshukuru Mungu kwa yote..

mapenzi ya siku hizi ni kuchungana kama ndama ... huwezi kuwa mbali hasa nje ya nchi ukategemea kukuta huku kuna usalama
 
Pole sana, si wasichana wote wako hivyo, ila nafikiri sio muhimu kufanya hivyo kwa msichana hasa ukiwa mbali.. Wengi yameshawatokea, either waliwasomesha au walituma PESA mingi kama wewe.. Mshukuru MUNGU na anza upya, MUNGU atakupa binti mzuri tena zaidi ya huyo....
 
pole mkuu...
uliweza kufanya maisha kabla ya kuwa na huyo binti!!
viyvo hivyo unaweza kuendelea na maisha yako baada ya kutoswa na huyo binti, koz hapo kabla maisha yalikwenda bila yeye...
mkuu samehe na sahau kuhusu yeye, maisha yatakwenda kama uyapangavyo...
 

Amin.! Nitazingatia yote..ukweli baada ya kuruhusiwa toka hospital, ilikuwa nigeukie maamuzi yasiyo salama ..kuna. kajihekima kadogo. Kalikobakia kufanya kazi ndani mwangu., ndo kannifanya kuwepo.au ni Mungu mwenyewe..asante kwa nasaha yenye faraja..nitaku-pm bdae ..
 

Thanx dada..hopefully will recover completely soon..!
 
ila pia si kila mtu atakuwa msaada kwako jaribu kuwa mchaguzi sana wa marafiki

BPM sijui kile kitufe cha thanks walikipeleka wapi
Huwa sometime nasema may be mimi ndo nafanya wrong choice au nini
Maana marafiki ni pasua kichwa nowadays hakuna tena wale marafiki walikuwa wanasema tuchanjiane damu au walio radhi kusema chako ni changu na changu ni chako
Siku hizi ni chako ni changu na changu ni changu na unafiki mwingi
 
........Pole,huna chako na anza upya kwani sasa atakuwa China,halafu katika kuanza kwako upya,fahamu pesa sio kila kitu katika mapenzi so kuwa kawaida sanaa!!
 

tatizo hatupimi matatizo na wala hatuna uhakika nani ndo msaada halisi kwetu .. tunapenda kushirikisha watu wasio sahihi na wengi wanapenda kusikia matatizo yako tu lakini hawana mchango wowote juu ya hilo tatizo hasa kwa utatuzi .. ni vyema hata kuleta jamvini utapata walau mwanga katika maamuzi.

marafiki wengi ni wanafiki umalizapo kumweleza tayari anatamani amiliki hata bbc kwa matangazo na anaweza kuongeza hata yasiyokuwepo
 
Truly! Nimeshaanza kulifanyia kazi jambo hili. Tnx

pia ni vyema ukashiriki mazoezi au matembezi au kutafuta sehemu ambazo kuna michezo ukaangalia inasaidia sana kupunguza stress .. ingewezekana kwenda beach ukapumzika na ukaanza kupanga mikakati ijayo kwani hutakiwi kuwaza yaliyotokea

"" jiepushe ulevi kwani hautakusaidia kukabili tatizo"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…