Ndugu Mtoa Mada.
Mawazo yote uliyopewa humu ni ya maana sana.
Mshukuru Mungu, huyo dada kaonesha tabia hizo kabla hamjaoana. Mabadiliko uliyoyaona ilikuwa ni Mpango wa Mungu wa kukuokoa ili usikumbane na dhahama ya badiliko la tabia wakati mkiwa tayari kwenye ndoa. Hilo lingekuumiza sana, na labda kupata mental breakdown. Una bahati sana Ndugu yangu. Shukuru kila siku kwa hilo kwani ni bora kumshtukia mchumba asiye Mwaminifu kuliko Mke wa ndoa asiye Mwaminifu. Zingatia (kama wewe ni Mkristo) ndoa haivunjwi kirahisi.
Jambo jingine; wewe ni kijana unayeonekana kuwa mwenye Elimu nzuri na umri wa kadiri. Ukijaaliwa kupata kazi, ni kipindi kifupi sana utarejesha unavyohisi umepoteza.
Jitahidi kutokuwa Mwenyewe. Kaa kwny vikundi. Badilishana mawazo na watu mbalimbali. Kamwe usikae mwenyewe, ni hatari. Jihadhari SANA na ulevi wa aina yoyote. Sikushauri ujiingize kwny mahusiano mapya ya kimapenzi. Kuna hatari ukaangukia pabaya. Subiri kidogo.
Natamani ningekuona lkn
Zingatia hayo kwanza.