Msaada wa ushauri/Nasaha..


Mkuu bahati mbaya tupo humu JF ila ingekuwa mtaani ningekualika sehem tuongee
Maana una ile idea marafiki walivyo siku hizi nisaidie na then ukishanisaidia au kunishauri huna tena thamani nami
Ndo marafiki wa siku hizi maana hata ukimweleza tatizo ushauri anaokupa ni wa kukuangamiza zaidi wala sio kukusaidia
yaani marafiki wamebaki ni wale wa kukutana club mnunulie bia na nyama choma piga story za wanawake na then kila mmoja aende zake hakuna la maana wala kushauriana
Ukimpata mmoja wa maana ni baada ya kuteseka miaka kadhaa
 

usijari mkuu ..
marafiki tuliona nao mradi ni rafiki lakini hatuna uchaguzi aina ya marafiki na ni muda gani nahitaji kukaa na rafiki .. wengi wetu watakuambia nina rafiki lakini kumbe ni kampani ya kwenda bar , kuongelea wanawake etc.. lakini rafiki ni yule ambaye unaweza hata akakushauri nini unatakiwa na nini hutakiwi katika maisha ya kila siku ( anachukua nafasi ya mzazi) na anatakiwa asiwe na haya katika kukurekebisha
 

Nimekupata mkuu..mvinyo situmii..
 

tatizo kubwa ni kwamba mkuu hawapo tena watu wa aina hiyo
tumebaki na kuwa na washkaji ambao tunakutana ijumaa kwenda bar kupata nyama choma na bia basi
Ila ukitaka ushauri jua imekula kwako
 
tatizo kubwa ni kwamba mkuu hawapo tena watu wa aina hiyo
tumebaki na kuwa na washkaji ambao tunakutana ijumaa kwenda bar kupata nyama choma na bia basi
Ila ukitaka ushauri jua imekula kwako

sasa mkuu rafiki wa bar si rafiki , rafiki ni yule akufaae katika dhiki na raha .. na hasa yule anayeweza kukupa muongozo hasa kimaisha , maana mwingine anaweza akakuambia mkuu umezidi sana mahudhurio ya bar punguza lakini hawa washikaji wa kukutana nao bar hataweza kukuzuia zaidi ya kutamani kila siku uwepo apate round
 
Duh!! Pole sana kaka, yaliwahi nitokea miaka miwili ilopita nikiwa Singida nafanya kazi, nilimpa binti kila alichohitaji, niliamini ndie angekuwa mke wangu, baadae nikahamishiwa mwanza kikazi ilibidi nimwache yy sgd ili nikaangalie khali ya upepo Mz, nikajashangaa kila nikim2mia nauri aje Mz haji! Badae akanipigia cm kuwa haniitaji ameisha OLEWA! Duh! Palikuwa pazito kiukweli, ila nilijipa moyo, nikaomba ushauri, nikatuliza kichwa. Baada ya miezi 5 Mungu akaniona, nikaondoka kuja Canada(nilipo sasa), binti nae akatimliwa na mme wake!! Akaja hadi kwa wazazi akimsingizia SHETANI ambaye hamjui sura! Nikamtosa! Hivyo ndg vumilia machungu, kaza roho, Fuata ushauri wa wana jf hapojuu, HAKIKA UTASHINDA! Ni mapito tu!! KATOSA, TOSA PIA!!
 

Umeongea mkuu na hilo ndio kubwa hapo kaka kuwa hakuna tena rafiki wa kukuambia hili ni baya au hili ni zuri
Wapo pale kusifia kuwa mfalme amependeza wakati yuko uchi
 
Pole sana mkuu.kwanza uyo mwanamke ulikutana nae mazngira gan?pengine ni hayo ya kujirusha c unajua maisha ya chuo.pia huna sababu ya kudai v2 ulivompa wala kulipza kisas kwan utaishia pabaya na kushndwa kuenjoy investment uliyofanya kwnye elimu muda mref.kuna quote moja wanasema '..find strenght and power then you wil enjoy the rest..'.so 2lia by nw na anza upya with fresh mind.mkumbuke mungu pia
 
Thank you bro. It's the hardest period of my life time. Nimejuta na kutambua kosa langu la kutotumia hekima aliyonijalia Mungu,labda yasingenipata..nyway, the xperienc and wisdom from Great thinkers here is highly inspiring.thnx.
 
sina la kusema kaka.nafsi inanisuta hapa..let me find again the strength and power,i hope will enjoy the rest. Great edvice
 
Ndugu zangu imefikia hatua sasa sitaki kujikubali na hali hii. Nimejitahidi kusamehe na kusahau, lakini ninashindwa..

Kwanini usiangalie upande wa pili na ukaona wewe ni mtu wa bahati sana? Kwa nini usione umepata ufunuo wa kwamba huyo bint hakufai? kwa nini unang'ang'ania kuangalia upande mmoja tu? Unataka dalili gani zitokee ili ujue wewe una bahati?
 
Pole mkuu kwa yote yalokupata, zaidi mshukuru Mungu kwa kukuonyesha mapema huyo binti ni wa namna gani. Napia imekukomaza pia kwa kukupitisha katika kipindi kigumu na kutambua kuwa ni Mungu ndo alokupa hako kaekima kadogo ka kujitambua na kufanya maamzi yaliyo mema ya kupiga moyo konde na kusonga mbele. Ni Mungu huyo huyo ndo atakaye kuinua na kukupa mke mwema na mali zaidi- songa mbele mambo yatakuwa shwari kaka.

You raised me up -by Josh Groban

you raise me up - josh groban with lyrics - YouTube


Josh Groban - You Raise Me Up (Video) - YouTube
 
pole sana mkuu mshukuru Mungu umepona kwenye ajali mbaya..........endelea kufanya shughuli zako sahau yote yaliyopita.......jitahidi kujichanganya na marafiki kuondoa msongo wa mawazo..........katika ulimwengu huu kuna matamu na machungu ni kipindi cha mpito wa machungu amini yatapita na maisha yatasonga mbele........usijihangaishe kumtafuta huyo dada atakuzidishia machungu
 
Kaka just take easy wengine tuliwahi kuwasomesha wachumba zetu wakatokomea hadi leo hii lakini maisha yanasonga na tumeshasahau.Chukulia kama vile umetoa sadaka tu na usije kulipa kisasi hata mara moja siku moja atakuja kujuta tu maisha ndio yalivyo usichukua uamuzi wa kijinga wa kulipa kisasi au kumfikiria sana kama ni muislam funga na kusali sana utasahu kama ni mkristo muombe mungu sana atakuongoza kwenye hiki ki[indi kigumu mimi yalinikuta last 4 years lakini now I happy family u cant even imagine.
 
Pole sana kaka, hizo ndio challenges katika maisha ya kimahusiano.
Jaribu kuukubali ukweli ingawa mchungu.
 
Umeongea mkuu na hilo ndio kubwa hapo kaka kuwa hakuna tena rafiki wa kukuambia hili ni baya au hili ni zuri
Wapo pale kusifia kuwa mfalme amependeza wakati yuko uchi

kama kinywaji kinakuja mezani unaweza kusifiwa hadi mwenyewe ukajiona mfalme kumbe wanataka round ya tbl
 

hapo inabidi aamini tu kapotelewa na pesa na mali ajipange upya maana malipizi hayafai ila mwenyezi mungu hulipa hapa hapa
 

kweli dada ulichosema masuala ya mahusiano apumzike walau si chini ya miezi sita ajipange aweze kufanya masuala yua maisha kwani wadada wapo atawakuta
 
Ha ha haaa, Mi nadaiwa simu kaka mpaka polisi tumefikishana
lakini nimetoa nje, eti haiwezekani lazima nimrudishie kisa hajawahi
hata siku moja...... upuuzi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…