tatizo hatupimi matatizo na wala hatuna uhakika nani ndo msaada halisi kwetu .. tunapenda kushirikisha watu wasio sahihi na wengi wanapenda kusikia matatizo yako tu lakini hawana mchango wowote juu ya hilo tatizo hasa kwa utatuzi .. ni vyema hata kuleta jamvini utapata walau mwanga katika maamuzi.
marafiki wengi ni wanafiki umalizapo kumweleza tayari anatamani amiliki hata bbc kwa matangazo na anaweza kuongeza hata yasiyokuwepo
Mkuu bahati mbaya tupo humu JF ila ingekuwa mtaani ningekualika sehem tuongee
Maana una ile idea marafiki walivyo siku hizi nisaidie na then ukishanisaidia au kunishauri huna tena thamani nami
Ndo marafiki wa siku hizi maana hata ukimweleza tatizo ushauri anaokupa ni wa kukuangamiza zaidi wala sio kukusaidia
yaani marafiki wamebaki ni wale wa kukutana club mnunulie bia na nyama choma piga story za wanawake na then kila mmoja aende zake hakuna la maana wala kushauriana
Ukimpata mmoja wa maana ni baada ya kuteseka miaka kadhaa