Msaada wa ushauri ninunue gari gani kwa bajeti ya 16M

Mkuu ukiwa huna uhakika na jambo ni vizuri sana ukanyamaza, I mean ukae kimya, hii ni busara zaidi, ikiwa unachoongea ni kweli sidhani kama production ya haya magari ingeendelea.
Tuwe makini sana
.
Hapo kwenye red umenichanganya mkuu, sijakufahamu kabisa
 
Hapo kwenye red umenichanganya mkuu, sijakufahamu kabisa
magari ambayo hayakufanya vizuri sokoni au yalikuwa na tatizo flani mara nyingi wanastopisha production. i.e brevis, starlet, verosa, mark11, chaser, etc.
 
renyo unavyosema ushawauzia sana discovery 4 na hawajaja kulalamika kwani inamaana gari zao zikisumbua ni lazima waje kwako .....waliotengeneza gari wanajua kuwa wamekosea ni kama nissan extrail generation ya kwanza hizi gari matatizo ya umeme sana na nissan walijua wakarekebisha to the next model ila ww unabisha ...kuna wauzaji na watumiaji ndugu
 
Kwa bajeti hiyo magari haya yatakufaa
-Rav 4
-Nissan Murano
-Kruger
-Harrier
-SUV NDOGO yoyote
Tena tafuta hapa hapa Bongo maana kuagiza hizo gari zitakugharimu zaidi

Mkuu kluger na Murano kwa 16m??
 
Sawa mkuu, but tatizo gari moja usi generalize kwa gari zote mkuu.
 
Toyata rav 4 old model ni gari ngumu and very economical. Ni zaidi ya escudo na barrier kwa mazingira hayo ya barabara zetu za shamba. Nunua hii kitu, hutojutia
 
Ni yard gani hapa daslam wanakouza Harrier, Murano na Kluger Tsh 16m?
Huwez pta harrier,murano au kluger kW 16 m toka yard labda used toka MTU binafsi tena yenye registration ya C kurud nyuma.Kama unaweza nunua Kluger yenye 4 cylinder ni gar ngum sana na mafuta sio kivile ila ukijichanganya ukanunua yenye 6 cylinder utajuta inavyomeza wese.Ukiwa na 23 m unapata yard
 
Nipe uzoefu wako kuhusu Discovery mkuu nmekua natumia sana Kluger but I wish kuibadil sasa
 
Niko hapa mkuu kwa magari bora na bei ya kitanzania.
Karibu Autocom Japan Inc
au pia waeza jiunga na group yangu katika whatsap amabyo nawapa ushauri watu na mambo mengine kuhusu magari,
Link Autocom Japan Inc

Weka number yako hapa nkutumie my phone number ili uniunge kweny hyo group
 
Suzuk vitara utakubali maisha mpaka mjukuu afu kamekaa kifamilia
 
Hizo hela zote wasaidie wagonjwa mahospitalini,,wasaidie vilema na wenye maisha magumu,,,..hakika utauona ufalme wa mbinguni
 
Barabara unayotumia ni rough road au rough???
 
Tafuta Rav 4 old model 1999-2000,au Harrier 4 cylinder old model ya 2000-2002
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…