MSAADA WA USHAURI WA BIASHARA BAADA YA KIFO CHA MMILIKI

MSAADA WA USHAURI WA BIASHARA BAADA YA KIFO CHA MMILIKI

Senior masai

Member
Joined
Jul 7, 2016
Posts
88
Reaction score
89
Habari wana jf
Nina complain moja kutoka kwa rafiki yangu
familia ilipoteza baba mzazi na walikua wana mradi wa mashine ya kusaga nafaka iliyosajiliwa kwa jina la kibiashara na kulipa ushuru na TAX CLEARANCE KILA MWAKA NA MAKADIRIO YA TRA pia baba alikuwa mzabuni katika shule kadha wa kadha katika mazingira walokua wanafanyia biashara,
baba alivopoteza maisha wakapitia wakati mgumu sana wa biashara sababu walipoteza na uzabuni katika zile shule zote,
shida ya sasa ni kwamba wanataka kubadili jina la biashara na kubadili umiliki kuwa wa mwana familia mwingine,
HOFU YAO:
Makadirio ya kodi yasiyoeleweka sababu wana familia hawana elimu ya biashara na makadirio ya kodi, pia Biashara haitoi faida yeyote saiv sababu eneo lipo crowded na mashine nyingi sana

Hofu ya kukadiriwa deni ambalo litakuwa halina ushahidi kwa upande wa anaedai wala anaedaiwa, {kulimbikiziwa deni bila ushahidi}

Mabadiliko ambayo hawayajui matarajio yake

MAONI YANGU KWA MASWALI YAO
Je kuna uwezekano wa kubadili jina la biashara au kampuni bila kujali taarifa za mmiliki wa nyuma? Kama itawezekana wafanye vipi? Wafanye usajili kama biashara mpya kabisa.

NITASHUKURU KWA MAREKEBISHO YA UANDISHI, NATANGULIZA SHUKRANI KWA MSAADA PIA
 
Sajilini jina jipya la biashara, na pia muwaandikie baruaTRA mkiambatanisha na nakala ya cheti cha kifo, ya kuwa mlipa kodi wao amefariki na hivyo wamtoe kwenye mahesabu yao.
Ingekuwa ni ishu ya mkopo wa benki kupitia dhamana ya majengo ya hiyo biashara, ndiyo kungekuwa na tatizo.

Nb: mimi siyo mtaalam wa biashara, au sheria.
 
Habari yako mkuu.
Baada ya mzazi kufariki, hatua iliyokua inafuata kwanza ni kiyeua msimamozi wa mieathi na hili hufanika mahakamani. Familia hukaa kikao, kama hakukua na wosia wowowte juu ya nani atakua msimaizi basi familia hupendekeza nani aww msimamizi.
Baada ya hapo huandaliwa muhtasari wa hicho kikao na maazimio husika kisha huenda mahakamani kufungua shauri lairathi.
Wakati shauri la mirathi linashughulikiwa mlipaswa kuteua msimamizi wa mda (receiver) wa biashara yenu, huyo msismizi kazi yake kwa wakati huo ni kuhakikisha anakusanya mapato yote ya biashara na kusimamia uendeshaji halafu anapaswa kuwasiliana na TRA kwa kuwaandikia barua (ahakikishe anakua na ushaidi wa kuwafikishia barua) kuwajulisha kuwa mteja wao fulani mwenye TIN namba fualani amefariki hivyo wapo kwenye mchakato wa kimahakama ili kumpata atakayekua anasimamia na kama kuna suala lolote basi wawasiliane na huyo msimamizi wa muda.
Baada ya uteuzi rasmi wa msimamizi wa mirathi toka mahakamani, huyo sasa ndiye atakua na mamlaka yote yaani KUKUSANYA, KUGAWA NA KUFUNGA mirathi ya marehemu.
Aliyegawiwa mashine(biashara) sasa anaweza kufanya mchakato wa kubadili umiliki.
Kuhusu suala la kubadili jiba la Kampuni ama Jina la biashara basi hayo yote yanawezekana lakini anayeweza kufanya hilo ni yule msimamizi wa mirathi ama yule aliyegawiwa mali husika.
Kuhusu TRA, mtakaa nao mezani muone kama kuna lolote hasa madeni yalikiwepo.

Kama biashara ni kampuni, basi HAKIKISHENI msimamizi wa muda anafika TRA haraka ili apatiwe credentials za E-FILING za marehemu ili aendelee kupandisha ritani za kila mwezi pamoja na makadirio ya mwaka huu kama muda haujaishaa.
Kila la kheri

0755963775 calls/whatsapp
 
Back
Top Bottom