Msaada wa Ushauri!!


Nashukuru sana nyamayao.Kwa kweli huyo mama ni mama wa nyumbani na hana hata kigenge chochote na hata huyo mwanaume kazi aliyonayo si ya kuweza kuhimili mahitaji ya kawaida ndo maana akawa amepangilia kwa kile kidogo akipatacho awze kuwahudumia hao wanne na huyo mama yao ambae hana hata kikazi cha kupika kwa watu.yaani wote ni wategemezi 100% kwa huyo baba.

Mtoto wa kwanza yupo Form IV ndo anajianda na mitihani,wa pili yupo Darasa la saba na wa tatu yupo Darasa la tano huyo wa nne ndo yupo chekechea.Wa kwanza mpaka wa tatu ni wanaume wakati huyo wa nne ni msichana.
Ndo hayo tu nyamayao
 
Mungu hawezi kukupa usichokiweza, yaani mtoto wa tano, amkubali na pia ni furaha na baraka kwa mama mkwe, asitoe ni dhambi, na pia akipende tu..atakuja kukushukuru kwa ushauri utakaompa.
 
Huyo mwanaume inaelekea ana mtizamo wa ki pro-choice. Mimi nina mtizamo wa ki pro-life na ushauri wangu unaegemea huko.

Ni vema akatafuta mbinu nyingine za kuongeza kipato ili kiendane na idadi ya watoto watano badala ya kuamua kutoa mimba. Alternatively, baada ya kumzaa anaweza kumpeleka kwenye vituo vya kulelea watoto yatima au aombe msaada kwa ndugu kama wapo ili wamsaidie.

Kama amedhamiria 'kuua' mmojawapo, ili abaki na wototo wanne, kwa nini asimuue huyo mkubwa wa kidato cha nne? Kutoa mimba licha ya kuwa ni kosa la jinai hapa tz, lakini pia ni hatari kwa maisha ya mkewe. Sioni ni vipi hao watoto wanne alionao wana haki ya kuishi zaidi kuliko huyo aliyepo tumboni.
 


nmekuelewa chaku......
 
Hili suala la kutoa mimba naomba mumchauri hayo mawazo ayaondoe kabisa. Anachokula yeye na mtoto atakula. Wampe tu uhai huyo mtoto mengine anajua Mungu. mara nyingi hizo huwa zinatokea sana unakuta mtoto wa mwisho ni mdogo wa kuwaita wazazi wake babu na bibi na hao ndiyo walezi wa nyumbani. Ndugu zake wakubwa watamuendeleza. Mungu ameipa hiyo familia uwezo angalau na amewapa jaribio la kupima imani yao kwa kuwaongezea mtoto.
 


sikiliza dada Kuna mimba nyingine zinaingia wakati mtu anatumia uzazi wa mpango iwe sindano au vidonge, na sijui ni kwa nini? kwa hiyo unaposema mama alizembea siyo haki.
cha kufanya wale mimba kumbuka wao wako kwenye ndoa kumtoa mtoto wa ndoa yenu ni vibaya , Mungu atawasaidia wamtunze na wamlee mziwanda wao.
Halafu hata kama huyo baba amepanga mipango yake tayari, sioni sababu ya kuchanganyikiwa kiasi hicho ina maana wana kipato kidogo sana au?
 

mtoto wao wa kwanza ataweza kusaidia na mdogo wake, kielimu nk ... pia, miezi minne si hatari kujaribu kuiondoa ??
 
Siyo sahihi yeye kumshauri mkewe kutoa mimba. Anamjali kweli mkewe? Je hajui madhara ya utoaje mimba? Mimi sidhani kuto kumtaka mtoto mwingine ni sababu tosha ya kumuweka mkeo umpendae katika risk. Kama yeye anaona huyo mtoto mtarajiwa ni tabu badala ya baraka aichukulie tu kama challenge nyingine ya maisha. isha tokea na hana budi kuonyesha uanaume wake na kuitunza familia yake. Ana weza kuona kero sasa but the baby could be a blessing to him, the family and to others.
 
Mungu hawezi kukupa usichokiweza, yaani mtoto wa tano, amkubali na pia ni furaha na baraka kwa mama mkwe, asitoe ni dhambi, na pia akipende tu..atakuja kukushukuru kwa ushauri utakaompa.

Mish,
Nakuunga mkono kabisa..na kwa kuongezea, hao wazazi wajiweke tayari kupokea majukumu yao kwa kile walichoshiriki kukiumba.Wasilaumiane na wasionyeshe huzuni kwa maana mtoto aliyeko tumboni hupata hisia hizo za kutokutakiwa na huja kumwathiri baadae.
 
Hili tatizo lipo sana bongo siku hizi. Mie nimewaona wamama wengi watu wazima wanatoa hizi mimba tena wanashirikiana na waume zao, ukiuliza sababu hawataki familia kubwa, mara watoto wanao wa kutosha, mara elimu kusomesha siku hizi tabu. Hadi mimba inaingia kwa nn hakuzuia? Na kama alishaona watoto wanatosha mie naona solution ni kutoa kabisa uzazi ili ubaki salama kuliko baadaye upate mimba halafu unamkatili mtoto wa bure na wakati alishaumbwa. Mwambie azae, then atafute mtu kwa kuadopt mtoto, kuliko kutoa hiyo mimba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…