Msaada wa ushauri

Msaada wa ushauri

Enoc jophrey

Member
Joined
Apr 28, 2015
Posts
24
Reaction score
5
Wapendwa wangu mimi ni mjasiriamali,natengeneza mashati ya vitenge, bazee, na batic. Kiu yangu kubwa ni kuhakikisha vazi hili la Africa linatamba.

Naomba ushauri wenu. Nataka niwe najumlisha katika maduka mbalimbali mikoani, je nini nifanye? Au kuna taratibu yoyote zinatakiwa? Naombeni ushauri wapendwa wangu.

Asanteni
.
 
Kwa dhamira uliyonayo jambo la msingi ni kuhakikisha unajitofautisha na wengine.

  • Mosi kuhakikisha unakuwa na nidhamu ya kazi.
  • Pili mbunifu.
  • Tatu muaminifu.
  • Nne kuamini elimu haina mwisho.
  • Tano kujitahidi kuwa na network pote ulipopalenga.
  • Sita kujitahidi au kubuni njia zitakazo kuwezesha kupunguza gharama za uzalishaji ili bei yako iwe "reasonable price". Watu wengi (mimi mmoja wao) bei zenu zinakuwa kikwazo kwetu.
 
Asante sana kwa ushauri wenye busara kubwa,nitafanyia kazi@Ngwananzengo
 
Back
Top Bottom