Kabla hujaanza tengeneza hizo katuni zenyewe kuna mambo ambayo ukijifunza kabla, learning curve yako itakuwa nyepesi.
1. Sketiching
Jifunze kuanda michoro ya kawaida kwa mkono. (Penseli au Pen ni sawa tu) kama animation zako zinaenda kuwa na watu halisi au wasio halisi, au wanyama, nk. Anza ujizoeze kuwa visualize kwenye karatasi.
2. Concept Art
Concept Art sana sana uhusika kwenye world building. Jinsi watu wakavyokuwa wakifanana. Au nyumba, magari, mazingira kiujumla yatakavyokuwa, nk. Mfano hizo katuni za Tom and Jerry hazifanani za Ben 10 au Soul(Pixar) au Coco, nk. Kila katuni zinakuwa na muonekano wake. Ko kwenye kufanya hizo concept arts unakuwa una define muonekano wa za kwako.
3. Character Design
Character Design hii ni nyepesi. Ni ile inayokufanya uone picha useme huyu ni Tom, huyu ni Jerry, huyu ni Spiderman au huyu ni Batman. Ina maana kila character ana vitu vinavyo mtofautisha na character mwingine.
Hayo yote ni mambo unafanya kwa karatasi.
Baada ya kujizoeza kuyafanya hayo yote. Unapaswa chagua unataka ku specialize kwenye aina gani ya Animations. 2D, Stop Motion au 3D Animation.
2D, ni animations ambazo zinachorwa kwa mkono, frame by frame. Animation za kawaida huwa ni 24F/s au 30F/s hii ikimaanisha michoro 24 ndani ya sekunde moja. Sikushauri kuanza na aina hii ya Animation maana inakuoaswa uwe mtaalamu kwenye kuchora , na mwenye muda wa kutosha. Mfano wa 2D Animations ni hio hio Tom & Jerry.
Stop Motion Animation, ni Animation zinazofanya kutumia vi midoli (clay figures) Yaani una unda characters wako, scener na kila kitu kwa mkono(kufinyanga) then unavianimate frame by frame kwa mkono uku ukipiga picha kila hatua. Sekunde moja itahitaji walau picha 30 ili animation yako iwe smooth. Sikushauri kufanya hii aina ya Animation kama ni beginner pia.
3D Animations ndo ziko za kisasa zaidi na ni rahisi kujifunza hata kama wewe sio mchoraji. Hapa inatumika software ku model kila kitu, kuanzia hao Characters, hizo Environments , na props. Pia software inatumika kuanimate kila kitu na mwisho wa siku render/export kazi yako ilokamilika.
Industry Standard softwares ni pamoja na Autodesk Maya, Autodesk Max , Maxon Cinema4D na Blender. Kwa kuanza nashauri kutumia Blender maana inakaribia kila kitu na ni ya bure. Pia ziko video kibao Youtube unazoweza tumia jifunza Basics hadi Pro stuff.
Baada ya kujizoeza software utakayochagua na kuwa vizuri kwenye kile unachofanya. Ni vizuri kuamua unaenda kuwa aina gani ya Animator(Unaweza kuwa vyote. But Animations bomba zinafanywa na Team, ambapo kila mmoja ana specificy kwenye kitu maalumu)
Kwa haraka haraka...
1. Unaweza kuwa Concept Artist - Huyu anasoma script na kuwavisualize hao character na sets zitakavyokuwa zinafanana.
2. Storyboarding Artist - Baada ya kujua kila kitu kitakavyokuwa kikifanana. Storyboard artist kazi yake ni ku visualize movie yote au film kwenye karatasi , scene by scene ili kusaidia Animators kujua flow itakavyokwenda.
3. Modelling Artist - Huyu ndie anatengeneza 3D Models za characters husika. Props na Mazingira.
4. Texturing Artist - Baada ya Models kutengenezwa, huyu Artist anahusika na kuzipa rangi/texture models husika.
5. Rigging Artist - Huyu anazipea skeleton hizo models ili ziwe rahisi ku animate.
6. Animator Mwenyewe - Huyu anachukua model ambayo iko rigged na kuanza kui ainamte, frame by frame(yaani sijui kufanya ka katuni katembee, au mdomo uongee, au macho yafumbe na kufuguka. Ni huyu).
7. Physics/Dynamics Artist- Huyu ndo analeta uhalisia kwenye hizo animations. Kama nguo kuperushwa na upepo. Kutengeneza upepo mwenyewe. Mvua. Mianga, Moto, nk.
8. VFX Artist - Huyu ni kutengeneza visual effects kama hizo nlizo taja hapo juu na zaidi. Muva, moto, radi, miripuko, vitu kubomoka, mambo kama hayo.
Ko unachagua skill moja wapo kati ya hizo na kuiendeleza kams uko sefiseriousous na kuigeuza hio kitu kuwa kazi, nk. Kam uko ambitious unaweza jifunze kuyafanya hayo yote. Inawezekana.
Goodluck