Kilimo Cha miti ya mbao ni uwekezaji wa muda mrefu kwahiyo hakikisha kuwa unafanya kwaajili Yako na warithi wako. Muda mfupi Kwa mti wa mbao ni miaka 15+ chini ya hapo lbda uitumie Kama Mirunda.
Kwenye kilimo ukubwa au udogo wa eneo haukufanyi upunguze majukumu, utafanya sawa na mwenye heka 5+. Yaani utalazimika kupalia, kuweka firebreak Kila mwaka, ulinzi dhidi ya mifugo na wezi n.k hivyo ongeza eneo au utafute mtu wa kusimamia kwaniaba Yako. Kuhusu aina ya miti watakujakuongeza ingawa gamsi inafaa inachukua muda mrefu, Kuna mipaina, n.k