Tatizo la msingi sio wasomi kutokuwa na ujuzi na weledi, tatizo kubwa linalotusumbua, mosi ni wasomi wenyewe na jamii kuamini hawawezi, pili ni uvivu. Mfano mzuri ni Rwanda, Rais Paul Kagame alikuja kachukua wasomi Wa Tanzania ili kuijenga Rwanda na kwa kiasi kikubwa wamefanikiwa. Ripoti ya shirika la kazi dunia (2013) ILO ilisema uwiano wa kazi kwa Mkenya na Mtz ni 1:5, kwa wazimbabwe ni 1:7,kwa watu wa EU ni 1:12. Hii tafsiri yake Mkenya 1 aweza fanya kazi ya watu 5 WATZ. Kuhusu misaada tatizo ni letu, kama rushwa na ufisadi tungevitokomeza ukusanyaji wa kodi ungepanda na misaada tusingeihitaji.