Msaada wadau! Mjukuu anagoma kwenda kozi ya unesi na ukunga Dodoma. Anataka kuendelea na kidato cha tano. Nifanyeje?

Msaada wadau! Mjukuu anagoma kwenda kozi ya unesi na ukunga Dodoma. Anataka kuendelea na kidato cha tano. Nifanyeje?

jnategemea huko advanc anaend kusomea nin,pcb ili iweje?
anageenda zake koz ya nursing dip tu kwaza anapata kaz na ka ana kichwa kizur anakuj badae kufanya Md bila shida na experianxe l!! shauri yake
 
Asome afike six Ni ufahari prestige kuwa na vyeti vingi vinavyoeleweka then ur Grandson/ Granddota Kama she or her still young Mwambie Asome Advance atapata Muda Mzuri wa Kufikiria Mambo mengi
 
Aende Advance. Akimaliza anakuwa na options nyingi za kuchagua.

Kama kuna Fani ambayo mtu anatakiwa aichague mwinyewe willingly basi ni nursing.
Tena akiwa wa kiume.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwache alafinywe na chand na Nelkon wiki 3 then ataomba mwenyeww chuo huyo.
 
Amechaguliwa kwenda chuo. Anasema hapana. Anatpenda aendelee na kidato cha tano kwa mchepuko wake uleule wa masomo ya sayansi. Wapi nigeukie ili nisaidiwe?
Aende chuo…… hana tofaut na anaesoma advance tofaut n kuwa yeye akimaliza anaeza pata kazi au kulamba deal bila kuwa na degree ila wa advance yeye mpaka asome degree

Uzuri course ya afya I wish ningekuaga yeye ……. Kuna watu wana bahati wanashindwa kuzitumia 🤦🏽‍♀️
 
Mshauri aende chuo.
Usiwe kama mdau hapo juu kumlazimisha asome kile wewe unataka, hayo ni maisha yake kikubwa wewe timiza wajibu wako.

Akiukataa uahauri wako wa kwenda chuo basi acha aende huko advance.

Ila advance sio salama sana kwa sasa, itambidi apige kitabu hasa ili walau fomlrm six atoke na kijiti ajichagulie chuo na course atakayo akipata hata 2 au 3 kupata chuo hasa hawa science kwa course wanazotaga wengi wao huwa ni changamoto.
Pia kupata mkopo kama wewe mzazi/mlezi uwezo huna, huenda elimu yake ikaishia hapo form 6 endapo akikosa mkopo na uwezo wa kumsomesha chuo mkakosa.

Kupanga ni kuchagua.
 
Hawa watoto sijui nani kawaloga eti kwenda form five kwao ndio dili. Nina uncle wangu mwaka jana alipangiwa chuo cha MUST course ya umeme eti akataka kubadilisha kwenda form five kashauriwa na baba yake, mimi nikamwambia wewe jaribu kubadilsha ndio utanijua mimi ni nani. Uncle akanisikiliza akaenda MUST kufika kule nikamuombea abadilishe course asome civil kwa sababu tayari kuna watu wamesoma umeme kwenye familia akapata. Leo hii ananipigia simu anafurahia maisha ya chuo na anatarajia kulamba hela ya IPT muda sio mrefu.

Kifupi watu bado hawaelewi kuhusu hizi elimu za vyuo vya kati wao wanadhani five na six ndio dili, hawajui zama zimebadilika.

Ushauri wangu kwako usikubali mjukuu akupande kichwani, mshauri umuhimu wa kwenda chuo tena uzuri ni chuo cha afya, tumia democrasia kumshauri ikishindikana tumia nguvu tena ikiwezekana mwambie akienda form five hutomlipia ada, atakuja kukushukuru baadae.
Sio sawa aisee, kwa upande wangu naonaa bora mtoto asome form five na six, ili aje apambane huko mbele mambo ya kumsotesha chuoni ambako anakutana na changamoto kama zote katika umri mdogo sio sahihi. tena bora hata Sayansi huku Arts ndio kabisaa kumpeleka akaanzie cheti ni uamuzi usio sahihi
 
Kusoma Advance kutampa nafasi ya kujitafuta na kuongeza bidii ili afaulu vizuri na aende chuo akapige zake MD au Engeering. Chuo sio pazuri kwani kuna peer pressure kubwa sana unampeleka mtoto wa 16 yrs anakutana na wenzake na wakubwa zake ambao wanamiliki vitu vya thamani na bata nyingine, tena ukute wana mkopo na yeye anategemea kila kitu kwako lazima alete wenge kwa kuijiongeza kwa namna anayoona inafaa ili aweze kwenda sawa na wenzake. Cha msingi mpe uhuru ila kumpeleka chuo sio suluhisho
 
Amechaguliwa kwenda chuo. Anasema hapana. Anatpenda aendelee na kidato cha tano kwa mchepuko wake uleule wa masomo ya sayansi. Wapi nigeukie ili nisaidiwe?
Mwaka 2015 nilipomaliza advance nilipangiwa nikasome PCM kiuhalisia niligoma kwenda serikalini maana nikiamini Hesabu siijui na nilipofuatilia uhamisho nilikosa,nikaamua Kwenda Advance kusoma PCB mason yalikuwa magumu kwangu hata siwezi Kueleza nachokumbuka baada ya kumaliza Form Five nikawaambia wazazi naomba niachane na advance niendelee na wazo langu la pili la kwenda chuo(Hivyo nikawa nimepoteza mwaka mmoja badala ya miwili)

Nikaanza chuo Kwa course ya Ordinary diploma in Nursing and midwifery kiuhalisia sikuipenda nayo pia maana Mimi nilitaka kusoma CO au Laboratory Ila nikaja kukubaliana na uhalisia wa Mambo nikiwa mwaka wa pili baada ya kuwa expert Wodini Kwa upande wa labour na General ward.

Nimemaliza chuo mwaka 2020 nimefanya kazi hospital kubwa Tu ya Serikali Kama internship na Kwa sasa nafanya Contract na Taasisi kubwa Tu ya research Kwa upande wa magonjwa.

Hivyo sijawahi kujuta Kuacha Advance maana Hata Hiyo diploma Nina GPA ya 4.5 so sina hata Haraka ya Kwenda Bachelor maana nimemuomba Mungu nikajisomeshe mwenyewe na si serikali.

Jamii bado Una Dhana ya advance na changamoto kubwa ya Advance Kwa sasa ufaulu imeongezeka Sana so Kwa mtu mwenye Division Two ni ngumu kusoma Course za Afya hasa Kwa Vyuo vya Serikali.

Ushauri wangu naombeni mmsimamie huyu kijana Aende uuguzi asije akawalaunu maisha Yenu yote baada ya Kwenda course za science na Kuishia kusoma Human resources and management.
 
Sio sawa aisee, kwa upande wangu naonaa bora mtoto asome form five na six, ili aje apambane huko mbele mambo ya kumsotesha chuoni ambako anakutana na changamoto kama zote katika umri mdogo sio sahihi. tena bora hata Sayansi huku Arts ndio kabisaa kumpeleka akaanzie cheti ni uamuzi usio sahihi
Darasa langu la Diploma.

Nusu ya Darasa walikuwa wametoka advance Nikiwemo Mimi Ambaye niliikimbia PCB...
 
Mshauri aende chuo.
Usiwe kama mdau hapo juu kumlazimisha asome kile wewe unataka, hayo ni maisha yake kikubwa wewe timiza wajibu wako.

Akiukataa uahauri wako wa kwenda chuo basi acha aende huko advance.

Ila advance sio salama sana kwa sasa, itambidi apige kitabu hasa ili walau fomlrm six atoke na kijiti ajichagulie chuo na course atakayo akipata hata 2 au 3 kupata chuo hasa hawa science kwa course wanazotaga wengi wao huwa ni changamoto.
Pia kupata mkopo kama wewe mzazi/mlezi uwezo huna, huenda elimu yake ikaishia hapo form 6 endapo akikosa mkopo na uwezo wa kumsomesha chuo mkakosa.

Kupanga ni kuchagua.
Watu bado wanaishi Kwa maisha ya mazoea Mimi nimesoma advance na nikaacha baada ya kuona naenda kufeli Tu na kupoteza muda.

Nikaenda kusoma course ya Nurse diploma na Nina GPA nzuri Tu,now nimeajiliwa na Taasisi nzuri Tu na Mshahara around 800K take home.

Degree nitasoma muda wowote japo miaka inaenda Ila sijapata sababu ya kurudi shule

Kuna Muda wazazi inabidi muamue ndoto za Watoto wenu hata kama kuna Mambo wanayapenda Sana.

Advance ya sasa Haiko kama ya zamani Demu wangu alipata PCB 1 8 akakosa MD mwaka 2017 akahairisha aende mwaka unaofuata akataka kukosa ndo nikamshauri akasome nursing now Yuko mwaka wa 3 bachelor.

So maisha yamebadilika Sana wakuu
 
Sio sawa aisee, kwa upande wangu naonaa bora mtoto asome form five na six, ili aje apambane huko mbele mambo ya kumsotesha chuoni ambako anakutana na changamoto kama zote katika umri mdogo sio sahihi. tena bora hata Sayansi huku Arts ndio kabisaa kumpeleka akaanzie cheti ni uamuzi usio sahihi
Mkuu hivi kati ya chet cha form six na certificate au diploma ya fani yeyoye ile kipi kinasoko? Cheti muhimu kwa upande wangu ni form four baada ya hapo mtoto akasomee fani kuanzia cheti, diploma kisha degree anaweza kwenda chukua akiwa kwenye ajira yake.Tena kwa issue ya ufundi anayeanzia cheti, diploma kisga chuo kikuu anakuwa fundi kweli kweli huwezi mfananisha na fundi aliyetoka form six akaenda chuo kikuu.
 
Back
Top Bottom