Msaada wadau wa CoET

Msaada wadau wa CoET

Muntu Ya Pori

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2013
Posts
222
Reaction score
64
Habari zenu. Nimechaguliwa Mechanical Engineering udsm ila mkopo nimenyimwa,so naomba kujuzwa ukitaka kuahirisha mwaka utaratibu ukoje? na kama unajiripia fdh zote kwa mwaka ni tsh ngapi. Na wapi naweza kuomba ufadhili wa kulipiwa gharama za chuo kwa makubaliano ya kuwafanyia kazi baada ya kufanikiwa kumaliza? naomba kwa yeyote mwenye msaad juu ya mambo hayo anisaidie,nimevulugwa mno na hawa HESLB
 
Ungeenda ofisi uwaulize jinsi ya kuanzika barua ya kuahirisha mwaka na kuhusu ufadhili bongo ni kitendawili kama taasisi kubwa (heslb) inashindwa itakuwa nyingine hapo mkuu komaa na ndugu
 
Hongera na pole , mimi nimemaliza mwaka huu 4th year hapo UDSM department moja na mechanical ,ukitaka kuahirisha mwaka lazima kwanza ufanye registration upewe kitambulisho hapo unaweza ukaahirisha hata miaka mitatu, unachotakiwa ni kulipa ada ya first semester 650,000 Tsh. na vitu vingine vidodogvidogo kama 75,000 Ths. hivi .Hapo utakuwa mwanafunzi wa UDSM na uamuzi unabaki kwako unataka uahirishe miaka mingapi
USHAURI
Kama utaweza kulipa hiyo ada apeal board,trust me unaweza kuletewa mkopo badae hasa kwa hiyo course yako,
na ikishindikana apply mwakani mkopo watakupa na hiyo ada utakayokua umelipa sahivi utarudishiwa mwakani
 
Back
Top Bottom