Nina ndugu yangu yupo kijijini, ni muhitimu wa kidato cha sita ameniomba nimwangalizie profile yake ya tcu...chaajabu nimekuta wame muekea kozi mpya zote tofauti na alizo ziomba, mfano udsm aliomba BA economics amekuta wamebadili wame weka BA in Fine and performning Arts, wakati yeye amesoma HGE na ana div 11, naombeni ushauri wana JF
dah anaweza pangiwa course ambayo hakuomba wala haijui, nilikuwa naomba ushauri wenu wa haraka.....je naweza msaidiaje huyu dogo kwa haraka? kabda awajatoa matokeo rasmi katika web yao, je akipata hiyo fine arts kuna uweze kano wa kubadili hiyo course na kurudi economics japo ni department mbili tofauti.... maana cutoff point zao alikidhi!
ndio maana tulikuwa tunasisitizwa kuwa hutembelee a/c yako ya tcu kila mara ili ujue kama kuna mabadiliko! Ila hapo hatakuwa kuna m2 kamfanyia mchezo mchafu cha kufanya ni kwenda kwny ofisi zao tcu
Mara nyingi huwa wanafanya hivyo kama kozi uli.zozichagua zote ziko priority na mkopo na hivyo kukupeleka kwenye non priority ili kuwe na sababu mbadala ya kukunyima mkopo kama heslb watathibitisha kuwa huna vigezo