Msaada wadau wiki la 41 bado hajajifungua

Msaada wadau wiki la 41 bado hajajifungua

chichimizi

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2015
Posts
1,074
Reaction score
339
Kama heading inavyojieleza hapo juu....

Habarini wadau jamani mke wangu anaujauzito na tarehe ya matarajio ilikua ni tarehe 1 lakini naona siku zinaenda tu mtoto wangu hazaliwi kazi yake nikurukaruka tu tumboni kwa mama yake.

Je hapa kuna shida gani?

Ushauri pls haina haja ya matusi
 
Kama heading inavyojieleza hapo juu....

Habarini wadau jamani mke wangu anaujauzito na tarehe ya matarajio ilikua ni tarehe 1 lakini naona siku zinaenda tu mtoto wangu hazaliwi kazi yake nikurukaruka tu tumboni kwa mama yake.

Je hapa kuna shida gani?

Ushauri pls haina haja ya matusi
Tulia kaka mbona hata 42 haijapita usiwe na wasiwasi just subiri kidogo
 
Mpaka raha wengine wakiambiwa mimba wanakimbia mpaka wanataka kuvunjika migongo,, hongera mno mkuu kwa hamu ya mtoto mengineyo yanatokea tuu kupitiliza siku
 
[emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122][emoji122]
Yaaani ni mekupenda bureee!

Wako watu hata kadi ya clinic haijui inaandikwaje!

Ndio hadi mtoto anakua hajui jina la baba kwenye kadi ni lake au kabambikiwa!

Kalenda ya mkewe ziroooo,akiambiwa Leo tarehe mbaya anakubaka tuuu utajijua mwenyewe, ukidungwa sindano ya uzazi , k imepoa imeloa
...........
Na wengine mengiiiii!
Hongereni wanaume wenye upendo wenye umakini!

Natamani wanangu wapate wanaume kama wewe!
Nakijana wangu najitahidi kimfundisha mapenzi ya ukweli,

I salute you chichimizi![emoji123]
 
Umri wa mimba ni siku 280 Sawa na wiki 40 kipindi ambacho kitaalamu huanza kuhesabiwa kuanzia siku ya kwanza ya kuingia hedhi kwa mara ya mwisho kabla ya kubeba ujauzito (LNMP - Last Normal Menstrual Period).

Bila shaka kinachokupa wasiwasi ni tarehe ya matarajio ya kujifungua (Expected Date of Deliver - EDD) ambayo pia huhesabiwa kutoka siku hiyo ya kwanza ya kupata hedhi yake ya mwisho kabla ya kubeba ujauzito.

EDD ni tarehe ambayo isikupe msongo wa mawazo kwa maana wapo wajawazito wakifikisha mimba ya umri wa wiki 36 huanza kujifungua kabla ya kufika wiki 40 na hujifungua Watoto waliokomaa. Wengi wao hujifungua kuanzia wiki ya 38. Mtoto alikomaa vizuri ni yule aliefikisha wiki 40.

Zipo sababu nyingi zinazosababisha wanawake kutofautiana kujifungua kabla ya wiki 40 baadhi ya sababu ikiwa ni pamoja na kufikia mwisho kwa Mfuko wa uzazi kutanuka.

Pamoja na kuwa umri wa mimba (Gestation age) ni wiki 40, ambapo pia umri huu huhesabiwa kuanzia siku ya kwanza ya hedhi ya mwisho kabla ya ujauzito, huwa kuna wiki 2 ambazo hupungua na kuwafanya wajawazito wengi kujifungua kuanzia wiki ya 38 na wakati huo huo wiki hizo mbili huongezwa hivyo kupelekea umri kikomo kuwa wiki 42 (siku 294).

Baada ya wiki 42 mifupa ya mtoto huanza kukomaa na kuwa migumu kupelekea kushindwa kuingiliana wakati wa kujifungua hasa hasa mifupa ya kichwa sababu ambayo husababisha uchungu pingamizi (obstructed labour). Lakini pia baada ya wiki hizo 42 kondo la nyuma huanza kuzeeka na hatimae kupunguza ufanisi wake wa kazi na hatimae kupelekea mtoto kukosa viini lishe, hewa kutoka kwa mama.

Hata hivyo suala la kukatisha mimba baada ya wiki 42 katika mazingira yetu bado ni changamoto maana utakuta baadhi wa wajawazito wanadai siku zimepitiliza lakini huwa hawakumbuki siku yao ya kwanza kuingia hedhi kabla ya ujauzito. Lakini pia wengine kalenda ni shida kwao kwa maana katika maeneo niliyopo mwanamke akiulizwa anadai wakati wa kupata hedhi hiyo ama kulikuwa kipindi cha giza au mbalamwezi. Lakini pia uchunguzi wa ultrasound nao bado kuna changamoto maana hii ni mashine inayoendeshwa na mtu na ndo maana ukipima ultrasound siku moja vituo vitatu au vinne utapata majibu tofauti tofauti.

Kufuatia changamoto hizo ndio maana hata baadhi ya hospitali au madaktari hawapendi kuanzisha uchungu au kuhitimisha mimba kwa hofu ya kutoa mtoto ambae hajakomaa (premature baby).

Kufuatia maelezo yangu hapo juu na kwa kuzingatia kuwa mkeo anao ujauzito wa wiki 41, naomba kwanza uondoe hofu maana hajafikia umri kikomo cha ujauzito. Lakini pia inabidi awe karibu na mtaalam wake kwa ushauri zaidi.
 
Una uhakika mtoto ni wako?? Maana takwimu za mwaka Jana tuliambiwa ety siyo wa kweenuu ..nakutania mkuuu usijekupasuka!! Hongera mwaya Muombe Mungu kipindi hiki huwa kigumu haswa kwa mkeo.pia kwasasa awe chini ya uangalizi wa daktari..BTW mtoto lazima atoke tu muda ukiwadia..andaa hela ya maana kama ni first born!
 
Umri wa mimba ni siku 280 Sawa na wiki 40 kipindi ambacho kitaalamu huanza kuhesabiwa kuanzia siku ya kwanza ya kuingia hedhi kwa mara ya mwisho kabla ya kubeba ujauzito (LNMP - Last Normal Menstrual Period).


Mkuu Ahsante sana sana kwa darasa hili natumai kaka yangu @chichimizi kapata elimu kubwa kupitia bandiko hili
 
Mimi wa kwangu alijifungua wiki ya 42
 
Kama heading inavyojieleza hapo juu....

Habarini wadau jamani mke wangu anaujauzito na tarehe ya matarajio ilikua ni tarehe 1 lakini naona siku zinaenda tu mtoto wangu hazaliwi kazi yake nikurukaruka tu tumboni kwa mama yake.

Je hapa kuna shida gani?

Ushauri pls haina haja ya matusi
Umechapiwa
 
Back
Top Bottom