Ni vyema ungetaja aina ya mic yako. Nimewahi kutumia condenser microphone aina ya BM-800 na nilipambana kama wewe katika noise cancellation. Nilifanikiwa kwa kufanya haya:
1. Kutumia wind shield/breaker ambayo imekuja na mic. Condenser mics nyingi huwa ni bi-directional, hivyo hukutaka kutumia windshield kwa lengo la kutuliza sauti unaporekodi kutoka upande mmoja, napo mazingira yawe yametulia haswa.
2. Tumia pop filter: ijapokuwa kazi kubwa ya hiki kifaa ni kukata plosives, filter pia itakusaidia kuondoa background/hissing sounds kwa mbali.
3. Tumia soundcard nzuri: nilinunua mic yangu na ikaja na “cheap USB soundcard” kama zawadi kwenye package yangu, sikupata matokeo mazuri ya sauti hadi nilipoibadili na kuweka soundcard mpya. Zipo nzuri, za aina anuai na kwa bei affordable tu.
4. Tumia Phantom Power: hii unaweza itumia kama mbadala wa sound card. Matokeo yake ni mazuri SANA kushinda ambavyo mic ingetumika na sound card, ila sasa gharama yake imesimama kiaina[emoji1]
5. Mwisho, japo si kwa umuhimu, tafuta mtandaoni software nzuri ya kurekodia sauti pamoja na settings zake zinazoendana na aina ya mic uliyonayo. Mimi, mathalani, ni mpenzi sana wa Adobe Audition lakini nilibadili kabisa uamuzi wangu baada ya kutumia muda mrefu kutafiti na kujiridhisha kuwa Audacity ina settings rahisi na compatibility kubwa endapo nitaitumia kurekodia sauti kwa mic yangu ya BM-800. Hapa noise cancelletion niliifanya kiulaini kabisa na nikatengeneza voice-overs babkubwa.
Jaribu ushauri wangu.