Msaada wajukuu wagombania ardhi je kisheria lipoje?

deo paul555

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2018
Posts
1,405
Reaction score
521
Wajukuu wanagombania aridhi,watoto wote ni wakiume yaani babu yao ni mmoja kasoro baba zao tofauti,kuna shamba lilikua lina milikiwa na babau yao alipofariki baba zao wakawa wanalimiliki hatimaye baba moja akafariki likawa linamilikiwa na baba yao mkubwa baadaye baba yao mkubwa akafariki sasa watoto wa mkubwa na mdogo wanarumbana kuhusu shamba hilo la babu yao kisheria likoje hilo msaada .
 
Kwenye mirathi alipewa baba yake nani kati ya hao wajukuu?
 
Kwa kawaida tunaanza na muhtasari wa shamba hapa tutahitaji copyright au hati miliki ya eneo huska,baada ya hapo tunakuja kwenye wosia hapa tutahitaji maelezo ya mwisho ya mmiliki hali wa eneo enzi za uhai wake je eneo aligawa kwa mfumo UPI kila Nyumba au alimpendekez tu MTU, hii ikikosekana basi Familia wanafungua kesi ya miradhi ambayo watampendekeza MTU wanaye muamini asimamie ugawaji wa eneo huska,kwa kawaida tuna mihimili mitatu ya ugawaji wa Mali 1.kimila 2.kiserikali 3.kiisilamu kwa mihimli hiz zote uwez tumia zote Bali mmoja tu,mfn mhimil wa kiserkal mm mkubwa unakuwa 1/4 ya ugawaji,mm wa kati 2/4pia kwa mhimil huu mwanamke ana haki ya kumili ardh,hapo kwa ufupi tu fungueni kesi ya miradhi na kila familia ipate gawio sahihi
 
Kama hakuna wosia wa kimaandishi uloachwa basi inabidi kiitishwe kikao cha familia/Ukoo kuchagua maimamizi wa mirathi na muktasari wa kikao Kisha waanze kwenda Mahakamani kulianzisha!
 
Hivi kuna urithi wa mjukuu kwa babu?????
 
Hivi kuna urithi wa mjukuu kwa babu?????

Upo!
Sasa Kama watoto wote wa babu hawapo unazani mrithi atakuwa nani?
Imeandikwa " mwenyeHaki ataacha urithi toka kizazi cha kwanza hadi 4 Kama sijakosea "
Sasa hapo unazani maana Yake ni nini?
Kwa hiyo siyo mjukuu tu bali hata kilembwe na kunyung'unya ana haki ya kurithi
 
maandiko ya biblia au sheria

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…