Msaada wako kwa huyu mdada tafadhali


Kamwambie pole sana kwa yote yaliyompata nawe pia pole kwa jirani yako na rafikiyo kapatwa na maswahiba hayo.Ukiwa kama rafiki yake jaribu sana kuwa naye karibu sana hasa kipindi hiki cha matatizo na uhakikishe kuwa asije kujaribu kutoa hiyo mimba.

Fikiria, kuna watu hawana watoto na wengine hawawezi kupata watoto kutokana na sababu mbalimbali ikiwa pamoja madhara yanayotokana na kutoa mimba. Siku zote mimba huonekana kuwa mbaya lakini matokeo ya mimba hiyo ambayo ni mtoto huwa kila mtu humkimbilia na kuonekana kuwa mzuri.Isitoshe tunahukumu wengine wakati pia nasi tunafanya hivyo hivyo kama huyo jirani yako.

Nani asiyekosea,nani asiye penda kusamehewa.Nani asiye fanya tendo la ndoa nje ya ndoa yake.Hakika kwa kuzingatia haya inatakiwa basi umshauri rafikiyo atunze mimba hiyo kwani ni muda wa miezi saba na nusu tuu ndiyo imebaki na atakuwa na mtoto.Wakati jamaa yake atakapo rudi ndo hapo kitakapo eleweka kwa wakati huo.Usijaribu kumtisha wala kumkatisha tamaa.Mpe pole sana nawe pia
Pole.
 
Wangwana acheni kuruka ruka na kujifanya watakatifu sana na mahakimu, kila mmoja wetu anajua jinsi sahihi ya kuclear hii mess ni kuitoa hiyo mimba full stop.
Aende hospitali kubwa inatolewa kitaalamu na usalama ni asilimia 99.9,

Wabeja mkulu
 
sasa moto ya mbongo humshauri kutoitoa mimba unafikiri nani atamtaka kati ya hao wawili huyo mwenye kibendi kaisha mtolea nje je akija huyo wa nje? Kama kufa ni siku yako imefika utakufa tuuu. Akatoe mimba.

Asante
 

Una busara sana
 
hakuna haja ya kutoa cha muhimu ni kujuta hiyo dhambi na kuacha kabisa kucheat. azae mtoto kumwua mtoto ni dhambi kubwa (kiumbe ambacho hakina makosa na wala hakiwezi kujitetea) akitoa atakuwa amefanya kosa kubwa. Mume wake akiamua kumuacha ajue ndio malipo ya hilo kosa.
 

mkuu dhambi ni swala la imani ambayo yeye anaonyesha hana kwa kitendo chake cha kucheat.
Hapo ni kuichomoa tu kunusuru ndoa na aibu ya kudumu for the rest of her life
 
mkuu dhambi ni swala la imani ambayo yeye anaonyesha hana kwa kitendo chake cha kucheat.
Hapo ni kuichomoa tu kunusuru ndoa na aibu ya kudumu for the rest of her life

Nyie watu hamuogopi kufa??
 
duu ndo utamu huo atalinywa keshalikoroga anywe tu
 
huyo mtoto atakaezaliwa aweza kuwa Rais wa miaka ijayo plz aache mimba azae kama msela atamuacha basi haikua zali lake maana anaweza kutoa mimba baadae akaja kukuta jamaa nae kazaa hukohuko nje ya nchi mie sishauri atoe mimba!huwezi jua huyo mtoto atakua nani hapo baadae!hata dini zinazuia utoaji mimba ni sawasawa na kuua pia hata wale watakaomshauri kutoa mimba watakua wameshiriki katika dhambi ya mauaji!
 
Sasa ameyaona matokeo ya kucheat tena na mume wa mtu,wakati anajua yeye ni mke wa mtu. Mimba asitoe ila asubiri mzee arudi moto uwake ikibidi amtaje na jamaa kwa mzee kwamba ndo mzigo wake!
 
Akatoe tu hamna cha kuzaa hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…