Mwenzetu
JF-Expert Member
- Dec 16, 2010
- 550
- 194
Nawasalimu tena kwa mara ya pili wakubwa shikamooni wadogo habari zenu.
Wakubwa naombeni msaada wenu wa mawazo,kuna mdada rafiki yangu na jirani yangu pia mumewe yuko nje ya nchi mie sikujua kumbe ana mwanaume anacheat nae,na ktk uhusiano wao mdada amepata mimba anataka aitoe ili kunusuru ndoa yake,alipomshirikisha jamaa anaecheat nae kuwa waitoe hy mimba jamaa kamjia juu sana na kumwambia hakuna kutoa na wala hajawahi kufanya hivyo! Ajabu sasa jamaa nae ana mke na watoto wanne!kwa sasa jamaa amesitisha mawasiliano yote ya simu na email hadi facebook kablock kisa hataki mimba itolewe,huyu mdada kachanganyikiwa alifanya siri lkn juzi kati hapa ilibidi anishirikishe kutaka ushauri,naombeni mawazo yenu juu ya huu utata wa hawa wenye ndoa.
Kamwambie pole sana kwa yote yaliyompata nawe pia pole kwa jirani yako na rafikiyo kapatwa na maswahiba hayo.Ukiwa kama rafiki yake jaribu sana kuwa naye karibu sana hasa kipindi hiki cha matatizo na uhakikishe kuwa asije kujaribu kutoa hiyo mimba.
Fikiria, kuna watu hawana watoto na wengine hawawezi kupata watoto kutokana na sababu mbalimbali ikiwa pamoja madhara yanayotokana na kutoa mimba. Siku zote mimba huonekana kuwa mbaya lakini matokeo ya mimba hiyo ambayo ni mtoto huwa kila mtu humkimbilia na kuonekana kuwa mzuri.Isitoshe tunahukumu wengine wakati pia nasi tunafanya hivyo hivyo kama huyo jirani yako.
Nani asiyekosea,nani asiye penda kusamehewa.Nani asiye fanya tendo la ndoa nje ya ndoa yake.Hakika kwa kuzingatia haya inatakiwa basi umshauri rafikiyo atunze mimba hiyo kwani ni muda wa miezi saba na nusu tuu ndiyo imebaki na atakuwa na mtoto.Wakati jamaa yake atakapo rudi ndo hapo kitakapo eleweka kwa wakati huo.Usijaribu kumtisha wala kumkatisha tamaa.Mpe pole sana nawe pia
Pole.