Wana JF, mimi ni mwajiriwa wa serikali! Nina mkopo wa tpb tangu mwaka jana, mikopo ambayo waajiriwa hudhaminiwa na mwajiri! Mwaka huu nataka niende kufanya Msc (ughaibuni), kwa mazingira ya ofisini kwetu najua sintakubaliwa! Kwanza ni kwa sababu hawana utaratibu wa kusomesha waajiriwa wao ktk ngazi za juu za elimu kama degree na Masters degree (hz roho mbaya zetu na chuki, hili hata sisi wafanyakazi tunalifahamu). Pili, kwa kuwa na mkopo ndio kabisaa, kikwazo cha wazi wazi! Sasa mimi nimeamua kujilipua (vijana wanasema kama mbwai mbwai). Nipo tayari kuondoka na kupoteza ajira yangu. Ushauri kama kuna madhara kisheria ambayo yatakuja kunicost mimi kama mwajiriwa ama familia yangu na hasa vitega uchumi ambavyo navimiliki (nina uhakika watajaribu kunifuatilia kutaka kujua kipi kinaendelea)!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.