Msaada wakuu namna gani Alibaba wanaship product kwa mteja

kwondeboy

Member
Joined
Dec 28, 2018
Posts
12
Reaction score
11
Rejea hapo juu mimi nimeamua kujihusisha na kuagiza bidhaa kwa jumla kwa wastani ambao si zaidi ya piece 50 kwenye product ndogondogo kama saa,usb n.k.

Naomba kujuzwa suala la shipping katika Alibaba linaendaje maana aliexpress unaposelect bidhaa wanakupa shipping option na bei yake lakini huku Alibaba sijaona kitu hicho wakuu.

Na alibaba vitu kwa bei ya jumla ndio cheap zaidi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jifunze Jinsi ya kufanya Manunuzi kwa Ebay mtandaoni - JamiiForums
 
Ata mimi nilikuwa napenda nifahamu vizuri kuhusu kuagiza mizigo alibaba sema ndo hivyo humu wengi wanabana hawataki kutoa connection
bado sielewi mzigo wa jumla inahitaji uwe na kiasi gan?
seller anaweza akaandika min order piece 50 lakini bado sielewi hizo ni sample kwanza au ndo mzigo wa jumla?
-
 
Rejea hapo juu mimi nimeamua kujihusisha na kuagiza bidhaa kwa jumla kwa wastani ambao si zaidi ya piece 50 kwenye product ndogondogo kama saa,usb n.k.
Ata mimi nilikuwa napenda nifahamu vizuri kuhusu kuagiza mizigo alibaba sema ndo hivyo humu wengi wanabana hawataki kutoa connection
bado sielewi mzigo wa jumla inahitaji uwe na kiasi gan?
TARATIBU ZA MANUNUZI ALIBABA NI HIZI
- Chagua bidhaa unayohitaji

1. Angalia sehemu ya mawasiliano na mawasiliano yafanyike ukiweka wazi
- Idadi ya mzigo unayohitaji
- Mahali mzigo unapelekwa
- Njia ya usafirishaji unayotaka itumike kulingana na ukubwa wa mzigo
- Njia ya malipo utakayoitumia

2. Atakupatia Quotation kulingana na hayo mliyojadili, utaipitia, na iwapo utalizika basi atakupa Performa invoice {Manunuzi + Usafirishaji hadi mahala aulipo} tayari kwa wewe kulipia

3. Utafanya malipo husika

4. Utasubiria mzigo wako uweze kufika nchini

5. Baada ya mzigo kufika nchini, taratibu za clearance zitafuata.

6. Utawajibika kulipia kodi /vat iwapo utatakiwa kufanya hivyo na mamlaka husika

NAKUTAKIA KHERI YA MWAKA 2019

www.bit.ly/101buy4me
 
sema ndo hivyo humu wengi wanabana hawataki kutoa connection
Ondoa hii dhana, Acha kuwa na mawazo hasi, Kuwa na mawazo chanya, Wengi wamefanikiwa na wanaendesha maisha yao kutokana na michango ya wana JF wengine.

Hakika JF hakuna kitu kinafichwa, Ni hazina ya kila kitu unachohitaji kufahamu.

Ili kupata jibu stahiki hakikisha
  • Unatumia jukwaa sahihi.
  • Hakikisha thread yako unaiandika kiukamilifu, kimpangilio wa kueleweka.
Na hakika utapata kile unachohitaji kufahamu.
 
case of alibaba hakuna shipping option kua watatumia DHL au free swali ni kua hapo inakuaje

Kwanza inatakiwa ufahamu tofauti ya wholesale and retail .

Aliexpress, ebay, amazon etl - Hizi zinaangukia kwenye kundi la retail store, Ambapo unakuta bei ya manunuzi na kusafirisha hadi kumfikia mteja.

Alibaba, DHgate, etl - Hawa ni Wholesale Suppliers
- Ni order toka kiwandani, Fuata tartibu hapo juu jinsi ya kuagiza.
- Inatakiwa uagize mzigo mkubwa,ambapo hutanguliwa na mazunguzmo ya kibiashara na muhusika masoko wa kiwanda husika.
- Bei wanazo ziandika ni FOB price ( Hapa inatakiwa ujue hizi terms FOB, CIF, EXW, CNF , ingia mtandaoni tafuta hizo terms), Sio bei utakayolipia kwa mzigo kukufikia.
- Huwa wanakubali pia kutuma bidhaa chache (moja au mbili) zikiwa kama sample na huhitaji wakusafirishie kwa njia ya haraka.

Nadhani umepata mwanga kutokana na haya maelezo kwa ufahamu wangu mdogo.

Karibu
 
Unajua maana ya alibaba??unaweza subiri mzigo mwaka
Ndugu
Je ni kwanini usubirie mwaka??

Sababu njia za usafirishaji ziko za aina mbili.
- Njia ya anga - Huchukua siku 7 hadi 14
- Njia ya maji - Huchukua wiki 4 hadi 7 kwa kutegemea ratiba ya meli inayobeba mzigo wako.

Iwapo utafuta taratibu sahihi za manunuzi mzigo wako lazima uupate kwa wakati, vinginevyo fedha yako inarudishwa.
 
Mkuu hujatafuta tu, mbona vitu karibu vyote viliisha jadiliwa humu, chimba mkuu kila kitu kipo humu humu JF.
 
nimejaribu kutaka kununu usb moja ya 16 gb dola 4 shipping fee wananiambia dola 25 hapa inakuaje?
 
Mkuu hujatafuta tu, mbona vitu karibu vyote viliisha jadiliwa humu, chimba mkuu kila kitu kipo humu humu JF.
Mkuu unajua huyu jamaa hapo awezi kupata seller ataesafirisha mzigo wa pieces 50 hiyo ni kama sample na wanaship kwa siku 5-7 na gharama zake za kuship zinakuwa mara nne ya mzigo ni hasara mana wanatumia dhl mimi nilikuwa nataka nijue minmu order ni kiasi gani kuagiza mzigo na wakakubali kuship kwa meli mana bidhaa nazotaka kununua zipo alibaba tu
 
nimeagiza usb moja ya 16 gb dola 4 shipping fee wananiambia dola 25 hapa inakuaje?
Ni sahihi
- Sababu wanatuma kwa njia ya express
- Ukitaka upate ghalama nafuu ambapo njia ya usafirishaji ni yakawaida angalia kwenye retail sites kama ALIEXPRESS, EBAY, BANGOOD, GEARBEST na zingine.
 
gharama zake za kuship zinakuwa mara nne ya mzigo ni hasara mana wanatumia dhl mimi nilikuwa nataka nijue minmu order ni kiasi gani
Sahihi kabisa,
Alibaba ni rahisi iwapo unaagiza mzigo mkubwa , carton box kadhaa, na usafirishaji iwe kwa njia ya meli.

Site sahihi kwake ni volumebest. com

---------------------------------------------------
Update:
- Volumebest haiko hewani kwa sasa
 
Ni sahihi
- Sababu wanatuma kwa njia ya express
- Ukitaka upate ghalama nafuu ambapo njia ya usafirishaji ni yakawaida angalia kwenye retail sites kama ALIEXPRESS, EBAY, BANGOOD, GEARBEST na zingine.
mi naona
Ni sahihi
- Sababu wanatuma kwa njia ya express
- Ukitaka upate ghalama nafuu ambapo njia ya usafirishaji ni yakawaida angalia kwenye retail sites kama ALIEXPRESS, EBAY, BANGOOD, GEARBEST na zingine.

nimefanikiwa kununua bidhaa flan kwa majaribio na kupitia sred kadhaa humu nimeweza,swali langu baada ya manunuzi na confirmation zote sijaona option ya kumtafuta muuzaji ili nimjulishe kama nimelipia mzigo au it is not necessary ataona tu mwenyewe au wata ni email? nimeficha hizo details kuogopa jamaa zetu wasije wakatrace na kunipata kirahisi mana mijadala ya kumponda jiwe inatufanya tuishi kama digidigi
 
kumtafuta muuzaji ili nimjulishe kama nimelipia mzigo au it is not necessary ataona tu mwenyewe au wata ni email? n
Taarifa za manunuzi anazo kupitia sellers portal ya site husika.

Subiri ndani ya siku 2 hadi 5 muuzaji ataweka update kuhusu usafirishaji wa bidhaa yako.
 
Taarifa za manunuzi anazo kupitia sellers portal ya site husika.

Subiri ndani ya siku 2 hadi 5 muuzaji ataweka update kuhusu usafirishaji wa bidhaa yako.
shukran sana mkuu,nimejifunza kitu kikubwa sana,kad yangu niliifanya iweze kununu vitu mtandaoni mwaka juzi but nilikua nanunulia domaon name godady sio kununulia items,this time naweza kujikita kwenye manunuzi ya items long live JF
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…