Msaada wakuu

Msaada wakuu

Dhokwa

Member
Joined
Jan 24, 2024
Posts
31
Reaction score
43
Heshima kwenu wakuu.

Samahani wakuu, naomba msaada namna ya kuipata hadithi au mwandishi wa hadithi fulani iliyopata kuchapishwa hapa jukwaani. Hadithi hii nilipata kusoma hapa jukwaani hapo nyuma kitambo lakini nimesahau jina na pia mwandishi wake. Hivyo naomba mwenye kuweza kunipa link yake au jina lake au jina la mwandishi wake nitafurahi sana. Ok. Hadithi hii inahusu mapenzi kama ifuatavyo.

Hadithi inamhusu kijana moja aliyepata utajiri kupitia uchimbaji wa madini Nyamongo. Baada ya kuwa tajiri akawa anamtafuta mpenzi wake aliyekuwa anamsadia wakati wakiwa wadogo. Bwana huyu alimuoa huyu dada lakini akamtesa sana baada ya kumpata mwanamke mwingine. Mwisho ni kwamba alikuja kuugua ugonjwa wa kupalalaizi na huyu mke wake akaja kumsaidia baada ya watu wote kumtenga ikiwemo yule mwanamke aliyemfanya kumfukuza mke wake awali ambaye pia ni mpenzi wake toka utotono. Wakaishi Kwa furaha kwani alificha madini Kwa kuyachimba kwenye kiwanja chake.

Naitafuta sana hii hadithi lakini nimesahau jina lake na mtunzi wake. Lakini nahisi ni wewe ndiye uliyeipost humu. Kama unaikumbuka au kuijua tafadhali nikumbushe namna ya kuipata. Asante sana.
[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom