Dodoma moja
JF-Expert Member
- Jan 3, 2014
- 307
- 182
Naomba kufahamishwa kuhusiana na mtu kuwa na mawazo kupita kiasi, matokeo yake ni nini katika mwili wake kiafya.
Naombeni sana mnisaidie wakuu!!!
Naombeni sana mnisaidie wakuu!!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Naomba kufahamishwa kuhusiana na mtu kuwa na mawazo kupita kiasi, matokeo yake ni nini katika mwili wake kiafya.
Naombeni sana mnisaidie wakuu!!!
Utadata bure. Jifunze kukubali yale usiyoweza kuyabadilisha wala kuyacontrol. Na yale unayoyaweza, weka bidii kuyatenda na utafanikiwa.
Kukabiliana na msongo wa mawazo namna ya kuepuka na (stress)Naomba kufahamishwa kuhusiana na mtu kuwa na mawazo kupita kiasi, matokeo yake ni nini katika mwili wake kiafya.
Naombeni sana mnisaidie wakuu!!!
NJIA ZINGINE ZA KUKABILIANA NA MSONGO WA MAWAZO (STRESS) HIZI HAPA
Msongo wa mawazo ama stress kwa kiingereza, ni tatizo ambalo kwa bahati mbaya sana limeendelea kuwa kitu cha kawaida sana kwa wanaadamu katika zama tulizo nazo. Katika miaka hii tuliyo nayo, ni sahihi kabisa
kusema kuwa, takriban wanaadamu wote walio hai wamekuwa wakikabiliwa na tatizo hili.Kuna baadhi ya aina za msongo wa kimawazo, ambazo zinaepukika na nyingine ni ngumu kuziepuka ila unapaswa kujua jinsi ya
kukabiliana na shinikizo la msongo wa mawazo pale linapokukabili. Hapa ni baadhi tu ya njia zilizo rahisi ambazo unaweza kuzitumia kukabiliana na hali hii pindi unapojikuta umetumbukia ndani yake
1. Jifunze kusema hapana hii ni katika mambo yako binafsi au kazi yako, unaitumiaje hii hapana? Unajua maofisini kuna swala la kupeana vikazi visivyoeleweka hata vimetokea wapi, yaani hujamaliza hili unaletea jingine hata kama sio kazi yako sasa jifunze kukataa hizi kazi zisizo za kwako ili mradi tu mfurahishe tu. hivyo hivyo vitu vidogo vidogo ndivyo vinavyokuletea msongo wa mawazo.
2.Jiepushe na watu ambao mara nyingi wanakusababishia Stress, unajua ukikaa chini na kufikiria utagundua kuna mtu flani au kundi flani la watu ndo linalokuleta msongo wa mawazo, sasa kaa nao mbali kabisa.
3. Simamia mazingira yanayokuzunguka. Mazingira yanakuzunguka yanaweza kuwa sababu ya stress zinazokukumba, mazingira yapo nayozungumzia mimi hapa? njia unayotumia kwenda kazini au kurudi nyumbani ina foleni sana? hiyo nayo inawea kuwa sababu ya stress ulizonazo, lakufanya epuka matumizi ya
barabara kwa wakati huo, mazingira ya soko wakati wakufanya manunuzi ya bidhaa mbali mbali yanakupa stress? nenda katika supermarket maana kwa kiasi flani kuna utulivu na hali ya hewa nzuri
4.Epuka Hasira za haraka, kuna ya mambo yanayohusu dini,siasa au maisha yako binafsi huwa yanakupa msongo wa mawazo basi jitahidi kuepukana nayo katika mazungumzo yako ya kila siku kwasababu yatakupa
hasira na kukufanya ukasirike na hili hupelekea kuwa na msongo wa mawazo, ukiingia sehemu ukakuta watu wanaongelea swala hilo epuka nao ili usiweze kuchangia na kujikuta unaingia katika mgogoro wa nafsi
5.Tengeneza orodha ya vitu anavyotaka kufanya sikuhiyo asubuhi tu ukiamka, mara nyingi unapaswa kujua mambo ambayo ni ya lazima kuyafanya kwa siku ambayo unaianza ili ikifika jioni usiwe na viporo, katika orodha
yako tenganisha orodha hiyo kwa vitu vya lazima kufanya na vitu vya kawaida ambavyo hata usipovifanya hazitakuharibia ratiba yako. kujua kipi cha lazima ni moja ya njia kubwa ya kupunguza msongo wa
mawazo.Naomba niishie hapa kwa leo maana nimewaonjesha yale ninayoyajua na ambayo nimejifunza, swala la kuondoa msongo wa mawazo linapaswa kuangaliwa kiundani zaidi maana ni pana sana, hapa juu nimeongelea
kuepuka stress ambazo si za muhimu ila kuna swala la saikolojia ambalo kwa kadiri siku zinaendelea, tutaligusia.
Asante mkuu kwa maelezo yako, naomba unisaidie pia athari zake kiafya yaan mtu akiwa ana msongo wa mawazo atapata matatizo gani kiafya au matokeo yake ni nini?