Msaada wana JF naibiwa

Msaada wana JF naibiwa

Niajir mimi nikufanyie biashara yenye akili...lol! Siku zote usiajiri mtu asiyejua thamani ya hela kwenye biashara yako ataishia kukunawa tu.
 
Habari zenu wana jamvi hasa wajasiriamali wenzangu. Mimi nafanya biashara ya vipodozi pamoja na saloon ya kike lakini kadiri siku zinavyoenda sioni maendeleo na duka lipo sehemu nzuri ya biashara, ninavyoona ni kama niliyemueka pale dukani ananiibia sasa naomba ushauri wenu pia naomba kuelekezwa namna yakupiga mahesabu ya thamani ya vitu vilivyopo ili nijue nina hasara kiasi gani.
Nawasilisha msaada wowote nitashukuru.
For a close look of your bussines tafadhali piga mahesabu weekly...ikishindikana sana monthly!
procedure ni zile zile sales-purchases-expenses=net profit

kwenye total sales usisahau kutoa bidhaa zilizorudishwa...

kwenye total purchases usisahau kuchukua open stock+purchaes-closing stock+carriage inward-returns outward...
 
Kama ni Salon, anaiwezo wa kutumia then akanunua tena materials bila mwenyewe kujua, kwahiyo ww ukija utakuta vitu havijatumiwa tu
 
Pole sana. kiufupi ni kuwa unaweza usibiwe bidhaa, wanachofanya ni wao kuwa na mzigo wao na kutumia duka lako kuuza, kwa hiyo hata hizo software, sijui stock taking na mengineyo wadau wanavyokushauri havitasaidia. Siku hizi kuna maduka muuzaji anakuambia kabisa yeye anacho hicho unachokiulizia kwa bei nafuu nje ya duka. kaa mwenyewe kaunta ndio utashangaa mauzo yalivyo makubwa.
 
Ilishaletwa mada hapa Jf mtu mmoja analalamika kwamba kwa nini mahoteli yetu ya kitalii hayaajiri watanzania ila huajiri wakenya kwa wingi. Mtu mmoja akajibu kwamba watanzania hawaajiriki kwa sababu ni wavivu,na wadokozi.
Kwa udokozi na wizi kwa kweli watanzania ni wataalamu, mpaka jambia la IGP wamelikwapua! Kwa hiyo ndugu yangu wa duka la vipodozi, kama huwezi kukaa huko dukani mwenyewe, basi imekula kwako. Hata umweke ndugu wa damu au sijui nani, atakuchomoa tu!
Mimi binafsi ilinibidi nifunge hoteli yangu baada ya kuandamwa na wizi/ udokozi wa niliowaajiri. Wa kaunta alidokoa hela za mauzo, wa jikoni ndo kabisaa walijichotea mavyakula na kupeleka nyumbani.
Ukimkamata mmoja, anavyopiga magoti na kuomba! Nikaona isiwe shida nikafunga hoteli!

Nasikitishwa sana na jambo hili, sijui tutabadilikaje? Mungu atubadilishe.

Ndugu, pengine suala la "Mali bila daftari hupotea bila taarifa" linaweza kukusaidia hapa. Kama siyo kila siku basi kila mwisho wa wiki demand records/mahesabu ya matumizi na mauzo yote ya wiki hiyo, kisha wewe calculate faida/hasara pia hesabu mali zilozopo dukani. Kisha demand kupewa hela kama mahesabu yanavyoonesha. Usiache muda mrefu upiti manake umeshaambiwa watanzania wengi ni wabunifu sana katika mambo ya wizi.

Ikishindikana badilisha muuzaji.
 
Fukuza kazi huyo jizi, funga cctv camera itasidia kumuogopesha
 
Habari zenu wana jamvi hasa wajasiriamali wenzangu. Mimi nafanya biashara ya vipodozi pamoja na saloon ya kike lakini kadiri siku zinavyoenda sioni maendeleo na duka lipo sehemu nzuri ya biashara, ninavyoona ni kama niliyemueka pale dukani ananiibia sasa naomba ushauri wenu pia naomba kuelekezwa namna yakupiga mahesabu ya thamani ya vitu vilivyopo ili nijue nina hasara kiasi gani.
Nawasilisha msaada wowote nitashukuru.

Ndugu yangu pole sana. Tatizo lipo kwako na wala si kwa huyo uliyemuweka hapo dukani. Kama ulifungua biashara bila kujua namna ya kujua thamani ya bidhaa ulizonazo inawezekana kuna mambo mawili...

1. Hujaibiwa ila kilichopatikana sio expectation yako, inawezekana ulikisia faida kubwa kwa kuwa hukupiga hesabu.

2. Labda umeibiwa kweli lakini ni mbaya zaidi unapoibiwa huku ukiwa haujui umeibiwa kiasi gani.

Ushauri.

Tafuta namna bora za uendeshaji wa biashara zako na hapo ndipo utakapokuwa na uwezo wa kugundua faida ama hasara halisi katika biashara zako.

Kwa msaada zaidi ni PM.......
 
Oooh pole ndugu.
Kwa upande wa vipodoz ungekaa mwenyewe kama muda wa week hivi na ukajua average ya sales ya biashara yako kwa siku. pia ungemshauri huyo muuzaji wako aandike kila kitu anachokiuza na bei yake katika sales register. Pengine huuza under price ukamhukumu anakuibia kumbe la. Kuhusu upande wa salon Nakushauri ufung CCTV camera ambayo kwa muda wako utaweza fanya replay na kuona idadi ya wateja walotembelea hapo salon kwako.
Ni hayo tu ndugu
 
Back
Top Bottom