For a close look of your bussines tafadhali piga mahesabu weekly...ikishindikana sana monthly!Habari zenu wana jamvi hasa wajasiriamali wenzangu. Mimi nafanya biashara ya vipodozi pamoja na saloon ya kike lakini kadiri siku zinavyoenda sioni maendeleo na duka lipo sehemu nzuri ya biashara, ninavyoona ni kama niliyemueka pale dukani ananiibia sasa naomba ushauri wenu pia naomba kuelekezwa namna yakupiga mahesabu ya thamani ya vitu vilivyopo ili nijue nina hasara kiasi gani.
Nawasilisha msaada wowote nitashukuru.
Ilishaletwa mada hapa Jf mtu mmoja analalamika kwamba kwa nini mahoteli yetu ya kitalii hayaajiri watanzania ila huajiri wakenya kwa wingi. Mtu mmoja akajibu kwamba watanzania hawaajiriki kwa sababu ni wavivu,na wadokozi.
Kwa udokozi na wizi kwa kweli watanzania ni wataalamu, mpaka jambia la IGP wamelikwapua! Kwa hiyo ndugu yangu wa duka la vipodozi, kama huwezi kukaa huko dukani mwenyewe, basi imekula kwako. Hata umweke ndugu wa damu au sijui nani, atakuchomoa tu!
Mimi binafsi ilinibidi nifunge hoteli yangu baada ya kuandamwa na wizi/ udokozi wa niliowaajiri. Wa kaunta alidokoa hela za mauzo, wa jikoni ndo kabisaa walijichotea mavyakula na kupeleka nyumbani.
Ukimkamata mmoja, anavyopiga magoti na kuomba! Nikaona isiwe shida nikafunga hoteli!
Fukuza kazi huyo jizi, funga cctv camera itasidia kumuogopesha
Habari zenu wana jamvi hasa wajasiriamali wenzangu. Mimi nafanya biashara ya vipodozi pamoja na saloon ya kike lakini kadiri siku zinavyoenda sioni maendeleo na duka lipo sehemu nzuri ya biashara, ninavyoona ni kama niliyemueka pale dukani ananiibia sasa naomba ushauri wenu pia naomba kuelekezwa namna yakupiga mahesabu ya thamani ya vitu vilivyopo ili nijue nina hasara kiasi gani.
Nawasilisha msaada wowote nitashukuru.