Msaada wana JF

mamkindi

Member
Joined
Mar 14, 2012
Posts
61
Reaction score
5
Msaada kwenu wana jf. nina tatizo la kupata maumivu kwenye vidole vya miguuni na mikononi na huwa joto linakuwa kali sana hata nikimshika mtu kwa mkono anaona nina joto ambalo siyo kawaida. swali ni kwamba nina upungufu wa damu au tatizo la mishipa ya damu? kwa yeyote anayeweza kunipa majibu sahihi na ushauri maana huwa inanitokea mara kwa mara.
 
Pole watalaam watatoa ushauri mzuri,uwe jirani kujibu hoja au maswali. Ilikupata ufumbuzi wa tatizo lako,uwe makini na wale makanjanja wanaokuja na kejeri.
 
naona possibility ya mambo matatu either una hyperthyroidism kwamba homoni za thyroxine zimezidi hivyo metabolic rate yako imeongezeka, au nahisi una gout kwa sababu ya maumivu vidoleni and less likely utakuwa unapata panic attack.
 
naona possibility ya mambo matatu either una hyperthyroidism kwamba homoni za thyroxine zimezidi hivyo metabolic rate yako imeongezeka, au nahisi una gout kwa sababu ya maumivu vidoleni and less likely utakuwa unapata panic attack.

Naomba ufafanuzi kidogo hapo kwenye hyperthyroidsm na panic attack
 
hyperthyroidism ni kwamba kiwango cha thyroid hormone ni kikubwa mwilini na ambayo kazi yake ni kuchocheo uunguzaji wa chakula ili kuleta joto japokuwa tatizo hili uambatana na sign nyingi kama vile macho kutoka nje na kuonekana makubwa na watu wengine hupata goita, panic attack ni kwamba mtu akiwa katika mazingira fulani hupata uoga mkubwa wa ghafla hivyo kufanya joto la mwili kupanda. hope it is useful!.
 
ila naona uangalie sana kuhusu gout kwa sababu tatizo hili huathili san vidole, another thing ni kwamba mtu akiwa na upungufu wa damu huwa wa baridi na sio wa moto so usihofu upungufu wa damu.
 
Nashukuru sana wadau kwa ushauri wenu, na nimeanza kufuatilia hospitali nasubiri kufanya vipimo ili kuweza kujua tatizo ni nini hasa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…