Msaada wanajamii

Msaada wanajamii

Parasite

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
613
Reaction score
575
Poleni kwa majukumu, samhani sana wadau naomba tena msaada wenu japokua ni kwa faida ya wengi.kwa kawaida tunafahamu kwamba kuna mizunguko ya hedhi[MENSTRUATION CIRCLES] mingi kulingana na tezi za mtu jinsi zinavyofanya kazi.sasa kuna dada zetu walishasema hapahapa jukwaani kwamba mizunguko yao inaenda hadi siku 34 alafu kuna hawa wenye mizunguko mifupi kama siku 22, 23, 24.

Sasa swali je? hawa wote siku zao zakushika mimba zinafanana au kuna tofauti? samahani sana naomba msaada wenu wanajamii.
 
Nenda kamuone Dr. Makumazeni, ye ndo mtaalamu wa hayo mambo yakinamama.
 
Kaka mimi haya makitu siyajui na wala sio demu lakini unashindwa kufikiria kuwa kama tarehe za mizunguko zinatofautiana siku ya kushika mimba itakuwaje ni moja?
 
nimechoka ntakujibu baadae nausingizi balaa
 
Aaaaaah! :angry::angry::angry::angry:
 
Chukua siku yenyewe eg 34 au 28 au 22 minus 15 utapata siku ya yai kuja kwenye uterus... mfano, mwenye 34 (34-15) atapata siku ya 19. Mwenye 28 (28-15) atapata siku ya 13. Mwenye 22(22-15) etc.
So kwa ufupi hawawezi kushika mimba siku zinazofanana!
 
nimechoka ntakujibu baadae nausingizi balaa
amu, ... Kweli una usingizi...??? Siyo kwwamba umeenda kushughurika na taratibu za hedhi...??? A.k.a kujipedisha...????
 
^^
Sasa, zikifanana unataka wazae watoto wa hulka moja.. Anyway JF DOCTOR watakusaidia
^^
 
Wanadamu hutofautiana sana katika fiziolojia. Kama ulivyosema kina mama nao wanatofautiana kwenye mizunguko yao ya hedhi. Kitu ambacho hakibadiliki ni muda wa kuachia yai (ovulation) kutoka kwenye ovaries kuelekea mji wa mimba.

Hii inatokea siku 14 kabla ya kuanza kutokwa na damu ya hedhi. Kwa mfano mwanamke mwenye mzunguko wa siku 21 basi ana-ovulate siku ya saba baada ya kupata hedhi yake, hali kadhalika mwenye mzunguko wa siku 35 ana-ovulate siku ya 21 baada ya kupata hedhi yake.

Ugumu upo kwenye kutabiri siku ya hedhi kwani nazo zinabadilika mara kwa mara, kwa mfano mwenye mzunguko wa siku 21 anaweza kuona siku zake kuanzia siku ya 19 hadi 23.
 
Ahsanteni sana wadau wote isipokua kuna utata kidogo kwasababu watu wengi hawajui hili swala ndiomaana ukiongea na vijana wengi utakuta mawazo yao yanafanana kila unaemuuliza anakwambia siku za neema ambazo mwanamke anaweza kushika mimba ni kuanzia siku ya 11-17 kutoka siku ya kwanza ya mzunguko wake.

Baada ya hapo hakuna tena hadi mzunguko ujirudie.sidhani kama mimi ni wakwanza kukumbana na vijana wa aina hii hebu ndugu zangu tusaidiane hapo.
 
Habari zenu,napenda sana madaktari ndo wazungumzie jambo hili kwasababu linaleta shida sana katika kufahamu kweli ya jambo hili.
 
Back
Top Bottom