Msaada wanaJF kila chakula nikila tumbo linavuruga na naharisha, nifanyeje?

ufumawicha

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2014
Posts
504
Reaction score
209
Hivi huu ni ugonjwa gani,maana leo naweza kuwa okay lakini kesho kwa chakula hichohicho nikaharisha vibaya.Madaktari wanadai niorodheshe vyakula vyote vinavyonisumbua na kuviepuka kwani hawaoni ugonjwa,tatizo laweza kuwa nini?
 
Tafuta dawa ulisafishe hilo tumbo lako mkuu, sijui dawa, ila nadhani inabidi uliflash lote
 
Pole jaribu kufanya detox/ unaweza pia tumia aloe vera gel ya forever nzuri sana kwa kusafisha kuponya na kusaidia tumb.....
 
Tafuta dawa ulisafishe hilo tumbo lako mkuu, sijui dawa, ila nadhani inabidi uliflash lote

Bulldog,naomba unisaidie namna ya kuflash tumbo maana sijawahi kusikia hiyo tiba.Kwa jinsi ninavyohangaika niko tayari siyo tu kuflash bali hata kulifua tumbo lote kama kweli hiyo itakuwa ndiyo tiba.
 
Mimi si mtaalamu wa madawa ila nadhani ukienda hospital unaomba wakupe dawa ya kusafisha tumbo lote, au MziziMkavu anaweza kutusaidia
 
Last edited by a moderator:
Hivi huu ni ugonjwa gani,maana leo naweza kuwa okay lakini kesho kwa chakula hichohicho nikaharisha vibaya.Madaktari wanadai niorodheshe vyakula vyote vinavyonisumbua na kuviepuka kwani hawaoni ugonjwa,tatizo laweza kuwa nini?
Pole Sana na mimi pia ninakuambia uorodheshe vyakula unavyo kula huenda unakula vyakula vingi vyenye Asidi vinavyokuletea matatizo ya Tumbo lako kuchefuka tuletee maelezo ya vyakula unavyo kula.

Mimi si mtaalamu wa madawa ila nadhani ukienda hospital unaomba wakupe dawa ya kusafisha tumbo lote, au MziziMkavu anaweza kutusaidia
Vipi ndugu hujambo?
 
Pole Sana na mimi pia ninakuambia uorodheshe vyakula unavyo kula huenda unakula vyakula vingi vyenye Asidi vinavyokuletea matatizo ya Tumbo lako kuchefuka tuletee maelezo ya vyakula unavyo kula.

Vipi ndugu hujambo?

Sijambo mkuu, saidia ndugu.

Halafu nina shida ya sikio, sijui uchafu umeziba? Nasikia kwa mbali sana.

Naomba dawa ya kuyazibua.
 
Tatizo linaweza kuwa ni food intolerance ambayo inaweza sababishwa na sababu kadhaa kuna kitu wanaita IBS hiyo huwa inaangaliwa kwa dalili tu haipimwi na haijulikani chanzo chake ni kipi

ni type ya digestive disorder, mara nyingi wanatibu dalili tu, labda ujaribu ku orodhesha ni vyakula vipi vinakusumbua kwanza...
 
Vyakula vinavyonipa shida ni nyama aina zote,wali,maharage,ndizi,samaki,dagaa,soda aina zote,mboga za majani kama chinese,matembele na mchicha.
 
Vipi kuhusiana na maziwa fresh, kahawa, chai, Alcohol havikupi shida hivyo mkuu? na vipimo ulivyopiga hospital ni vipi? sasa kwa maana hiyo ni vyakula gani ambavyo vikawa angalau kidogo? na tatizo hilo lipo kwa muda gani? na dawa gani ulishawahi kuzitumia? Basi nijibu tuendelee...
 
Pole Sana na mimi pia ninakuambia uorodheshe vyakula unavyo kula huenda unakula vyakula vingi vyenye Asidi vinavyokuletea matatizo ya Tumbo lako kuchefuka tuletee maelezo ya vyakula unavyo kula.

Vipi ndugu hujambo?
acha siasa wewe unaesema aorodheshe vyakula anavyokulaga manake we huvijui vyakula vyetu vya ki tz. Hawezi taja bagga wala piza bana we kama unajua msaidie tu kuliko kuuliza vitu unavyovijua. Haya ugali na ubwabwa
 
hahahahaha udaktari si kazi ndogo aulizwe mwingine ujibu wewe
 
Back
Top Bottom