Msaada: Wanauchumi nitawezaje kusave mshahara wa laki moja na ishirini, ili nami niwe na mafanikio?

ku-save hiyo ni ngumu sana mkuu, kwa kipato cha milioni moja kwa mwezi unaweza ku-save angalau elf 50 kibishibishi, na hapo inategemea kama huna ndugu na marafiki wa kupiga mizinga.
 
Usijali kwa mshahara huo, wengi tulio humu ni watu wa kawaida tu sema id znatuficha.
Kwa maisha haya ya sasa ni ngumu sana kukwambia utasevu pesa kutoka kwenye 120k ukilinganisha ba gharama za maisha ila usikate tamaa, cha kufanya tafuta mishe nyingne ya kufanya either kwa muda wa ziada baada ya kutoka kazini au upate kazi nyingne yenye kipato kikubwa zaidi ya hicho, ikishindikana fanya kujiunga na kikundi cha kikoba uweke 20k kila mwezi then baada ya mwaka tafuta hata bustani ulime.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ku-save hiyo ni ngumu sana mkuu, kwa kipato cha milioni moja kwa mwezi unaweza ku-save angalau elf 50 kibishibishi, na hapo inategemea kama huna ndugu na marafiki wa kupiga mizinga.
Milioni 1..! Mkuu endelea kuendekeza marafiki. Msimu huu wa sikukuu kazi yangu imekuwa kukusanya madeni yangu kwa nguvu; naiona 2020 ntakua na marafiki wachache sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu unataka u save ufanikiwe kwenye nini kama ni maisha ni ngumu kutoboa na huo mshahara
 
kuku wangu alitaga mayai kumi na mbili lakini alitotoa vifaranga 9, mayai mengine yaliharibika.
safari ijayo akitaga tena 12 basi matatu nitayala kwa ugali.

Hasara Umfika Mwenye Mabezo
 
Mkuu, nakushauri utembelee jukwaa la biashara na usome zile nyuzi kwa utulivu sana.
Huo mshahara ni mdogo sana, kwa ku-save ni ngumu tuongee ukweli. Jaribu kubuni biashara ndogo ya mtaji mdogo ambayo haina risk kubwa. Yaani ikilala au ikikaa sana isile kwako sana. Kuna mdau kasema unajitolea kufundisha, kama ni kweli wauzie ubuyu na karanga wanafunzi wako. Kwa kuanzia utakuwa unalaza kati ya 5,000.
Kipato kikiongezeka, na wewe buni wazo jipya.
 
Hiyo pesa ndogo mno aisee. Labda uwe na shughuli nyingine baada ya muda wa kazi rasmi kuisha.
Kama unafanya ualimu kama unaweza anza kupigisha pindi baada ya vipindi wanafunzi wakulipe hata 200 kila kichwa. Ukipata tu vichwa 25 una 5000 kila siku.
Hasa ongea na wale wa vidato vikubwa. Muhimu jiweke karibu na tengeneza urafiki na wanafunzi wakukubali.
 
Dah mkuu nimejarib kubana ili uishi bila kuchanganyikiwa lakini natoka patupu.Mbinu zangu zahitaj usiri wa hali ya juu ila.Mbinu yangu itakufaa ikiwa utahitaji kutoka kwenye iyo kazi yaani ujiajiri au upate chanzo kingine cha kukuongezea kipato.

*Kwa mshahara wako kubali urudi nyuma kapange nyumba iliyo jirani na kazini ili uende kwa miguu ofcn na kupunguza gharama za usafiri ikabid panga nyumba ya kiza kuondokana na gharama za umeme simu utachaj 200 vibandan.

*Punguza gharama za simu toka mb na dk utumie sms tu naamini haitazid 1500 kwa mwezi (kifurushi cha mwezi)

*Kula 1500 kwa siku yaani 1000 mchana uwapo kazini na 500 usiku Chai na kitafunwa (utapika nyumban mana chai mgahawani usiku utaonekana mchawi)

*Achana na habar zote za starehe ziache tu zikupite.

*Kuhonga iwe ni mwiko nalo hili ni gumu kuliko ila ukiwa karibu na mungu ukawa muumin hakika hili utalishinda.

kumbuka yote hayo unayoyafanya sio kuepukana na maden bali upate akiba sio yakuongeza thaman ndani au kubadil smartphone bali kubadili kazi kujiajiri au likawa gumu kujiajir basi kupata kazi ingine ya ziada itakayokuwezesha kuongeza kipato.

#Kwa mchanganuo hapo juu nimepata
Kod ya nyumba 30000 umeme na maji

#Chakula 1500*30=45000+ 5000(Sukar majani)= 50000

50000+30000=80000 ( yaweza kupungua ikiwa utapanga nyumba ya kiza)
80000+10000(vocha(sms)+sabuni+ usafir wa dharula nk)
90000 kwa mwezi.
120000-90000=30000
30000 ndiyo akiba ambayo utaitumia kutengeneza mtaji wa biashara ingine na dharula kama kuumwa nk)

Kama nakuona utakavyo taabika pia vibarua na vikazkaz vya mtaani usijivunge jichanganye.Binafsi nimeishi kwa gharama ya 60000 kwa mwezi.
Kod 20000+5000 umeme maji hayazid 1000(200 dumu)
Kula 1000 kwa siku amazing story (nilikunywa chai na maandazi au mara moja moja na kufunga swaum za Sunnah nakufutur msosi wa 1000 jioni) Sifanyi kazi ngumu.
26000+30000=56000/= Iyo 4000 hapo 1500 vocha sms ndio kuwasiliana no kupiga,2500 dawa mswak+ sabuni+mafuta.
Nikutie moyo nalipa kod 80000 (chumba na sebule) frem za kaz baada ya kuongeza mtaji now nalipa 200000 kwa mwezi (frem 3).Nabadili mlo nitakavyo sio tena chai maandazi na kufunga swaum.

Bado napambana na haya maisha so ubahili ndio maendeleo yalipo.

Mtangulize Mungu na Fanya mambo kwaajili yako usiseme watanionaje akina fulani niliosoma nao.
Kila la kher na afya ndio mtaji wako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mmh mshahara 120k..Kodi,maji,umeme,mavazi,nauli na Kuna kuumwa..hiyo pesa haitoshi mkuu ni vyema ukatafuta chanzo kingine Cha pesa na Kama una mwanamke ni vyema akusaidie katika utafutaji auze hata vitafunwa..adamke alfajiri aende ilala(kama mko dar) akajumue mitumba atembeze..pambana mkuu usikate tamaa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata bando hili la kuchati huku atakuwa anapigwa tafu sio ? Hahahahahahah nimependa mahesabu yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…