Msaada wapi naweza pata mbegu nzuri ya vifaranga vya kuku

Msaada wapi naweza pata mbegu nzuri ya vifaranga vya kuku

pettymarcel

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2012
Posts
2,161
Reaction score
880
Wapendwa katika bwana, mimi natarajia kujikomboa kiuchumi kwa kujikita katika ufugaji wa kuku wa kienyeji chotara baada ya kupata mafunzo wengi kutoka kwa wataalam mbalimbali kutoka kwa kubota, mama joe, livapul fc, mama jimmy gazet,kichwa mbovu na wengineo sasa nimeona ni muda wa kutake action mim nipo mkoan kilimanjaro moshi naomba mnisaidie wapi nitapata mbegu nzuri nataka kufuga chotara kwa ajil ya mayai na nyama nitaanza na vifaranga 200 plz nisaidien wakuu sitaki kutembea na bahasha tena nataka nipambane mpaka kieleweke kwanini kubota aweze mimi nishindwe no thanx nitapambana aisee
 
Fuatilia mabandiko kama haya humu na pia unaweza fika Ruvu Jkt kama uko jirani ma maeneo hayo
 
unataka wa One day old, au wa wiki moja, Mbili, Tatu au mwezi, ila moshi na rusha nadhani si mali so unaweza wapata Arusha,
 
Ningepata wa mwenz ingekuwa vema zaidi vp waweza nielekeza wapi mkuu na bei zao?
 
Nipo arusha nina kuku kama aina tatu {1} light sussex hawa wananyama nyingi na hutaga mayai mengi pia wanavumilia sana magonjwa {2} nina kuku wekundu wa izrael wakubwa sana na wazito (3) nina kuku weusi wa malawi na wamayai ya blue pia karibu sana
 
Mimi ninmashaka na hawa wa Israel, wekundu kwa sababu nilio waona mimi kenya ni pure Kienyeji, waati hawa unao wazungumzia ni kama wa kisasa make hawaatamii, na kenye ile taasisi ya Kenya rangi yao si hii nyekundu bali ni rangi kama Kanga ndege au madoa doa,
Hawa wekundu wanaweza kuwa ni wa kisasa lakiniwametoka Israeli kwa sababu Israeli hakuna Aina moj ya Kuku, kumbuka wale watu waliwahi hadi kutengenezea kuku maabara ambaye hana manyoya kabisa, ila ni kuku na anatembea, yuko Uchi

So ninao zugumzia mimi ni Pure Kienyeji, n wapo na wengine kutoka South Africa kwa Wazuru ambao nao ni mbegu nzuri sana na ni Pure
 
kitomari sasa hao wa kwanza (light sussex) wa siku moja ulisema unauza sh.2000/= je wakiwa na wiki moja au wiki mbili au wiki tatu au mwezi mmoja unauzaje? Na je wana chanjo tayari? Mimi nataka chotara.
 
makaruka machotara wangu wa sku 1 wanakua teari na chanjo ya mareks
 
makaruka machotara wangu wa sku 1 wanakua teari na chanjo ya mareks
Mkuu kama hutojali naomba ufafanuzi wa hawa kuku wako wa susex maana inaonekana ni wa uwekweli sana kibiashara
1)wanachukua siku ngapi mpaka kukomaa na kiutosha kutaga/kuingia sokoni??
2)Vipi wanastahimili magonjwa??
3)Wanataga na kuatamia au wanataga wenyewe???
 
wanataga wakiwa na miezi 4 nanusu tu hutaga mayai mengi sana na wananyama nyingi sana
 
Hao Susex vifaranga unauzaje Mkuu?

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
kifaranga wa cku 1 ni elifu 1 na miatano wa mwezi ni elfu 300

Hebu tuweke rekodi sawa. Kifaranga wa siku moja ni sh. 1500/= na hao wa mwezi ni sh. 3000/=?! Sawa au sivyo. Sasa kutoka Arusha kuja DAR inakuwaje? Funguka bro kitomari2.
 
Hahaha,huyu kitomari wenu anaongea kwa mapozi kama vile si mfanyabiashara.
Weka details zote,bei,contact zako na physical address ulipo,sio watu wanakumbembeleza afu unajibu kimkato kama hutaki vile.
 
Back
Top Bottom