Msaada: Wataalam wa maji

Msaada: Wataalam wa maji

Faana

JF-Expert Member
Joined
Dec 12, 2011
Posts
38,657
Reaction score
44,759
Naomba kusaidiwa
Nimejenga water tower yenye height ya mita 3.5 nimeweka tank la lita 5000 inlet line size yake ni robo tatu na outlet line size yake ni inchi moja na nusu, water tap ni 4 za (2 za nusu inchi na 2 za robo tatu) lakini changamoto ni kiasi cha maji yanayotoka kwenye water tap hizo ni kidogo sana hata kama nikifungulia tap moja tu yanachuruzika, fundi amehangaika ameshindwa.

Shida inaweza kuwa wapi
 
Shida ipo kwenye size ya outlet line, nchi 1½ ni kubwa

Kawaida hapo huwa inawekwa unequal tank connector ya nchi 1 kwa ¾ inch, halafu huku chini tena inawekwa reducing socket ya ¾ inch kwa ½ inch kabla ya kuifikia water tap. Kadri size ya bomba inavyopungua ndivyo presha ya maji inavyoongezeka

Ramani, Makadirio au Ushauri tuwasiliane
 
Naomba kusaidiwa
Nimejenga water tower yenye height ya mita 3.5 nimeweka tank la lita 5000 inlet line size yake ni robo tatu na outlet line size yake ni inchi moja na nusu, water tap ni 4 za (2 za nusu inchi na 2 za robo tatu) lakini changamoto ni kiasi cha maji yanayotoka kwenye water tap hizo ni kidogo sana hata kama nikifungulia tap moja tu yanachuruzika, fundi amehangaika ameshindwa.

Shida inaweza kuwa wapi
Zingatia ushauri wa comment #2.

Yaani kifupi yaingize kwa bomba kubwa, yatoke kwa bomba dogo ili kutengeneza msukumo mkubwa wa kutoka.

Mf: yaingie kwa bomba la 3/4 yatoke kwa bomba la 1/2.

Kama utaona ni shida ama ni hasara kuezua hayo mabomba ya awali, hakikisha kabla ya kufikia tape unaweka redusing toka bomba ulilotandika awali kuja 1/2 ili kuyabana yapate kasi ya kutoka.
 
wadau wameeleza nilichotaka kusema. huyo fundi ni kanjanja amacha kwenye fani.
 
Zingatia ushauri wa comment #2.

Yaani kifupi yaingize kwa bomba kubwa, yatoke kwa bomba dogo ili kutengeneza msukumo mkubwa wa kutoka.

Mf: yaingie kwa bomba la 3/4 yatoke kwa bomba la 1/2.

Kama utaona ni shida ama ni hasara kuezua hayo mabomba ya awali, hakikisha kabla ya kufikia tape unaweka redusing toka bomba ulilotandika awali kuja 1/2 ili kuyabana yapate kasi ya kutoka.
So nafanyaje kusahihisha kosa kama tank connector ya kutoa ni 1 na nusu, imetembea urefu wa mita 4, ikawekwa reducing socket ya 1 na nusu to 1 inch then 3/4, kisha ikatembea umbali wa mita 12 hivi ikawekwa tap mbili za 3/4 na 2 za 1/2
 
Maji yako yanatembea umbali mrefu sana, na ukiangalia hata height ya mnara wako ni ndogo achilia mbali masuala ya bomba zilizotumika.
Factors zingine zinazochangia hilo tatizo ni pamoja ya position ya mnara wako ulipojengwa, umbali wa water tap zako kutokea kwenye mnara
 
Back
Top Bottom