Kwa kawaida battery inapimwa kwa Ah unakuta 100Ah (Ampere Hour) Kwa lugha nyepesi unaweza tumia taa ya 10 Watts ikachukua masaa 100-120 kwa battery kuisha charge. Battery za Solar zinapimwa kwa Ah na sio N. mara nyingi za N zinatumika kwa magari na vifaa vya moto.
Battery umesema unahitaji heavy duty ila nadhani ni kwamba unahitaji zenye kukaa na charge muda mrefu. Nikushauri hivi kwanza jua matumizi yako ya umeme ni watts ngapi kwa siku baada ya hapo ni rahisi kujua unahitaji system ya ukubwa gani kwa sababu si battery tu utahitaji kubwa Solar,Charger controller vyote vinafaa kuwa calculated kulingana na matumizi yako. Unaweza kufanya kienyeji ila Battery zitakufa baada ya muda mfupi sana.
Pannel zinavyokua kubwa tambua ndo zinavyotumia muda mfupi kujaza battery zako. Ukiwa na pannel kubwa jua la 1hr linatosha kujaza battery zako umeme wa kutosha kutumia 24hrs. Ila unapokua na Panel ambazo ni ndogo kuliko battery zako ni kwamba inatumia muda mrefu sana kwa Battery zako kujaa na hii itakuathiri sana kipindi jua si zuri au hakuna jua kabisa (Usiku) utajikuta ikifika sa mbili usiku umeme umeisha kwa kuwa mchana battery hazikujaa moto.
Majibu ya swali lako ni haya 60A solar charger controller, 12V 600AH battery au hizo N100 zako ziwe 6 ziungwe in Series. Ukitumia Battery chini ya nilivyokushauri hazitodum zaidi ya miaka 2 zitakufa.
KUMBUKA: Hata battery iwe nzuri kiasi gani utaiua kwa kuizidishia mzigo/load isiouweza.
Nimeandika haraka haraka ila nadhani utaelewa tu.
Kila la kheri