Msaada Wataalamu wa Kiswahili, matumizi ya haya maneno ambayo hunichanganya

May Day

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2018
Posts
6,311
Reaction score
9,027
Lipi ni neno sahihi kwa matumizi.

Maneno kama Yuko na Yupo, Wapo na Wako, Sipo na Siko, Tupo na Tuko, Uko na Upo.

Baba yuko nyumbani au Baba yupo nyumbani.

Kesho sipo nitakwenda Moshi au Kesho siko nitakwenda Moshi.

Leo tupo Kanisa la Arusha Mjini au Leo tuko Kanisa la Arusha Mjini.

Kaka upo nyumbani nije? au Kaka uko nyumbani nije?.
 
.
20220114_054101.jpg
 
Kiswahili ni kama lugha nyingine kubwakubwa.Mara nyingine tunaongea kwa misingi yake,kwa mazoea au uasili wa mtu ana(ko)poishi ili kuwasiliana vema na kuelewana.

Niliwahi kutaka kuongea kiswahili kwa kanuni, misingi na ufasaha nikajikuta naongea bila mtiririko mzuri, kigugumizi, na kuwa kama naongea huku naota. Si hivyo tu. Nilianza kuongea kama mgeni wa lugha au mtoto anayejifunza. Mkuu, weye ongea kwa kutiririka na kwa uhuru tu.
 
Kiusahihi wa matumizi, neno linaloishia na 'po' linatumika kwa kitu au kwa mtu aliyekaribu na wewe au na kitu fulani.

Mfano, 1. shuka lipo kitandani.
2. Mimi nipo sebuleni, watoto wapo barazani wanacheza.

Na neno linaloishia na 'ko' ni kinyume chake, yaani ni kwa matumizi ya kitu au mtu aliyembali na kila mmoja.

1. Alizeti iko Singida na Dodoma tu.
2. Viatu viko kwa fundi.
 
Kiswahili ni kama lugha nyingine kubwakubwa.Mara nyingine tunaongea kwa misingi yake,kwa mazoea au uasili wa mtu ana(ko)poishi ili kuwasiliana vema na kuelewana.
Niliwahi kutaka kuongea kiswahili kwa kanuni,misingi na ufasaha nikajikuta naongea bila mtiririko mzuri,kigugumizi,na kuwa kama naongea huku naota.Si hivyo tu.Nilianza kuongea kama mgeni wa lugha au mtoto anayejifunza.Mkuu,weye ongea kwa kutiririka na kwa uhuru tu.
Upo sahihi sana mkuu, ukifuata kanuni zake hutaweza kuongea kwa uhuru. Mfano, mzuri kwenye kiswahili hakuna neno linaloishia na 'ga' mfano naendaga, nalalaga. Ila husipoweka hizo herufi za 'ga' maongezi yako yanaweza kuonekana hayana mvuto!
 
Kijana wa Ngui na kiswahili sanifu...
 
Upo sahihi sana mkuu, ukifuata kanuni zake hutaweza kuongea kwa uhuru. Mfano, mzuri kwenye kiswahili hakuna neno linaloishia na 'ga' mfano naendaga, nalalaga. Ila husipoweka hizo herufi za 'ga' maongezi yako yanaweza kuonekana hayana mvuto!

"Husipoweka"
Usipoweka.
 
Kiusahihi wa matumizi, neno linaloishia na 'po' linatumika kwa kitu au kwa mtu aliyekaribu na wewe au na kitu fulani.

Mfano, 1. shuka lipo kitandani.
2. Mimi nipo sebuleni, watoto wapo barazani wanacheza.

Na neno linaloishia na 'ko' ni kinyume chake, yaani ni kwa matumizi ya kitu au mtu aliyembali na kila mmoja.

1. Alizeti iko Singida na Dodoma tu.
2. Viatu viko kwa fundi.
Shukran Mkuu.
 
Kiswahili ni kama lugha nyingine kubwakubwa.Mara nyingine tunaongea kwa misingi yake,kwa mazoea au uasili wa mtu ana(ko)poishi ili kuwasiliana vema na kuelewana.
Niliwahi kutaka kuongea kiswahili kwa kanuni,misingi na ufasaha nikajikuta naongea bila mtiririko mzuri,kigugumizi,na kuwa kama naongea huku naota.Si hivyo tu.Nilianza kuongea kama mgeni wa lugha au mtoto anayejifunza.Mkuu,weye ongea kwa kutiririka na kwa uhuru tu.
Upo sahihi kabisa ila mimi nionavyo lugha sanifu kwenye maandishi inapaswa kuwa makini zaidi ukilinganisha na ile ya maongezi, maana maandishi yanaweza kutumika sehemu tofautitofauti na kwa muda mrefu...na huweza kukukera hata wewe uliyeandika pale utakapogundua ya kuwa ulikosea baadhi ya maneno.
 
Back
Top Bottom