Kwa faida ya wengine pia hili suala la mawazo ya biashara naona linakua kwa kasi sana na hii siwalaumu sana wanaoomba mawazo ila hakuna mfumo mzuri wa kutoa elimu ya biashara kwa wale ambao watahitaji kufanya biashara, Wazo la biashara huwa sio kitu cha kuomba upewe na mtu mwingine ila liboreshwe na mtu mwingine na hakuna mtu asiekuwa na wazo la biashara,kila mtu anawazo lake la biashara lakini aidha unaliogopa au unaliona ni kubwa kulifanya, nitatoa sababu kwanini sio sahihi kuomba wazo la biashara ila kuomba liboreshwe.
1. Kila mtu anamawazo yake na kila mtu ananjia zake za kufanikiwa hivyo iwapo utaomba wazo mtu atakupa wazo ambalo aliliwaza kwake litamfanikisha au ni wazo ambalo analiona litafanya kazi kwake, lakini sio kwaajili yako ni yake atakwambia anachowaza kitaweza kufanya kazi kwake hivyo mfano: ukisema una milioni 20 na unatafuta wazo la biashara. Ataiweka katika mipango yake na uwezeshaji wake ikitosha atawambia lakini ni tofauti kwako.. wewe ukisema milioni 20 unategemea fresh idea na ambayo itakuwa na watu ambao wanajulikana ili kufanya nao kazi lakini kiuhalisia unapoanza ni lazima uanze kidogo kidogo na kutafuta sehemu ambazo gharama ni nafuu ili kupunguza gharama za kurasmisha hivyo mpaka hapo itakuwa iko tofauti sana na wewe japo linaweza kuwa wazo zuri lakini sio la kwako, la kwako unalo kichwani aidha unaliogopa au unalidharau.
Kaa chini jisikilize fuata taratibu za jinsi ya kupata wazo la biashara kisha anza kulifanyia kazi,usitafute pesa kwanza ndio ufikirie wazo la biashara, pata wazo kwanza halafu pesa itakuja kujaza kulingana na wazo lako na uhitaji, mfano unasema una milioni 20 ukapata wazo la kufungua biashara kariakoo frem ni mil 3 - 7 kwa mwaka, kuitengeneza iwe kama unavyotaka milioni 2 - 5, kununua biashara yenyewe milioni 5 - 15, kulipia ada mbali mbali?kumlip wa kukusaidi kazi?,Bado biashara haijaingiza hasara? mwanzo biashara huwa hailipi ila unailipa,utajikuta umepoteza kila kitu. Kwa maelezo zaidi kuhusiana na jinsi ya kupata wazo la biashara na ujasiriamali tembelea elishachuma.blogspot.com au humu humu JF kwa jina la Elisha Chuma utapata elimu itakayokupa mwanga wakuanzia.