Natafuta gari ambayo inauwezo wa kubeba watu 7 au 6, na yenye uwezo wa safari ndefu katika barabara zetu za Tz. Nina mpango wa kutumia gari yenyewe kwa miezi mitatu tu na nimeshauriwa kuwa gari aina ya Toyota Noah inafaa. Nimepata fununu kuwa mtaani bei ni kati ya ml. 8 na 10 na showroom ni kati ya ml. 13. Je gari ya aina hiyo kwa ml 8-10 inatakiwa iwe imetembea kilometer ngapi? na kwa hizo za showroom zinatakiwa ziwe zimetembea kilometer ngapi kwa bei hiyo? Je uuzikaji wake baada ya matumizi ya muda huo unakuwaje?(mtumiaji makini) Gari za aina hiyo ni ngumu katika kuuza? Nilitaka kukodi ila nikashauriwa kuwa kukodi kwa miezi mitatu itagarimu kuliko kununua na kuuza. Naomba ushauri ikiwa pia kuna aina nyingine ya gari ambayo inaweza kuwa inafaa zaidi ya noah( ukizingatia bei matumizi na uuzikaji wake baada ya matumizi)
Natanguliza shukurani zangu.
Natanguliza shukurani zangu.