Msaada: wazoefu wa magari naomba ushauri

Msaada: wazoefu wa magari naomba ushauri

chosti

New Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
3
Reaction score
0
Natafuta gari ambayo inauwezo wa kubeba watu 7 au 6, na yenye uwezo wa safari ndefu katika barabara zetu za Tz. Nina mpango wa kutumia gari yenyewe kwa miezi mitatu tu na nimeshauriwa kuwa gari aina ya Toyota Noah inafaa. Nimepata fununu kuwa mtaani bei ni kati ya ml. 8 na 10 na showroom ni kati ya ml. 13. Je gari ya aina hiyo kwa ml 8-10 inatakiwa iwe imetembea kilometer ngapi? na kwa hizo za showroom zinatakiwa ziwe zimetembea kilometer ngapi kwa bei hiyo? Je uuzikaji wake baada ya matumizi ya muda huo unakuwaje?(mtumiaji makini) Gari za aina hiyo ni ngumu katika kuuza? Nilitaka kukodi ila nikashauriwa kuwa kukodi kwa miezi mitatu itagarimu kuliko kununua na kuuza. Naomba ushauri ikiwa pia kuna aina nyingine ya gari ambayo inaweza kuwa inafaa zaidi ya noah( ukizingatia bei matumizi na uuzikaji wake baada ya matumizi)
Natanguliza shukurani zangu.
 
Kilometer huw zinachezewa, si hoja.

Tafuta dereva mzoefu wa hayo magari uende ukajaribu nae. Na prefer dereva mzoefu kuliko mafundi wa bongo, atakupa tathmini nzuri ya hilo gari.
 
Kilometer huw zinachezewa, si hoja.

Tafuta dereva mzoefu wa hayo magari uende ukajaribu nae. Na prefer dereva mzoefu kuliko mafundi wa bongo, atakupa tathmini nzuri ya hilo gari.

Ushauri wako mzuri.
Tatizo:
Baada ya matumizi ya miezi mitatu kwa sasa hivi soko la Magari Tanzania ni gumu kidogo. Kipindi cha Uchaguzi mkuu watu walikuwa na njia nyingi za kupata pesa, lakini kwa sasa hivi matundu mengi yamezibwa, yamebaki machache ambayo hata hivyo hayavujishi vya kutosha.

Sina maana ya kukukatisha tamaa, ila kukuandaa kwani unaweza kubahatika kupata mteja au ikachukua muda. Wabongo wanapenda vitu cheap, ukianza kutaja mamilioni 7 na kuendelea si wengi waliotayari.
 
Mimi nina toyota hiace nina mpango wa kuifanya daladala ndio nimeishaifanyia clearance...bado sijapata namba nyeupe kwa ajiri ya biashara ina namba za kawaida..kama unaiitaji kwa hiyo miezi mitatu na upo serious tuwasiliane,kununua gari na kuliuza utakula hasara..hautauza kwa bei unayotaka wewe...sasa nipo dubai ila gari lipo kigamboni..kama upo serious tuwasiliane..+971504374387 dubai...wawezapia ku pm
 
Nashukuru kwa ushauri wenu, nitazingatia wakati wa kufanya maamuzi.
 
Back
Top Bottom