Msaada wenu kuhusu android Radio za kwenye gari

kalanga1

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2017
Posts
318
Reaction score
432
A. alaykum, za leo ndugu zangu?

Naombeni msaada wenu, mimi nataka nifunge Android redio kwenye gari pamoja na zile Tv za nyuma ya siti lakini nashindwa kujua kampuni ipi ni bora na ipi ni fake, nimejaribu kwenda kariakoo nimepita kuuliza zinacheza kwenye laki na nusu hadi laki na 80.

Nikija mtandaoni hawa wanaojitangaza wanaanzia laki 3 sasa nashindwa kujua lipi ni lipi. Sasa kwa mwenye uelewa wa hizi radio anielekeze niangalie kitu gani ili nijue ipi ni nzuri na ipi ni fake?

Au kwa walio funga tayari kwenye magari yao waje hapa wanipe ushauri wakati wa kununua niangalie kitu gani na gani, au wanielekeze labda walipo nunulia kwa bei nzuri na OG na mm nikapate.

Ahsanteni sana.
 
Mimi sijui kuhusu hizo radio zinazouzwa hapa madukani hapa dar. Pia hujasema gari yako ni gani?

Ushauri wangu, kama unaweza kujilipua agiza Radio specific ya gari lako Aliexpress au Alibaba kuliko kununua Universal ambazo zimejaa humu madukani.

Faida.

1. Radio specific inafit exact kwenye gari yako. Haitokezitokezi pembeni.

2. Utapunguza kukatakata wires wakati wa kufunga radio. Gari ikishakatwakatwa wire hicho ni chanzo mojawapo cha shoti na mwisho gari kuwaka moto.

3. Unaweza kupata radio yenye specifications kubwa kuliko kutoa laki tatu halafu unafungiwa radio ina 1G ram na 16GB of Storage.

Kazi kwako mkuu.
 
Asante sana. Umefafanuka vizuri sana ndugu yangu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…