Hali ya kitenzi kuhitaji yambwa inaitwa kitenzi elekezi : kwa mfano, mtoto analilia. Kitenzi ni "analilia" moja kwa moja ni hali ya kitenzi kutoweza kukamilisha taarifa mpk kuwepo na neno au maneno yakukamilisha. Ktk mfano huo inaweza kuwa " mtoto analilia u
Hali ya kitenzi kutohitaji yambwa inaitwa kitenzi si elekezi. Kwa mfano " dada anacheka", "kaka analia" "mtoto amelala". ktk mifano hiyo vitenzi ni anacheka, analia, na amelala. Unakutana na vitenzi vya namna hiyo hupati maswali kichwan khs taarifa inayozungumziwa moja kwa moja uanaelewa.
Kwa kuongezea kuna kitu kinaitwa vitenzi elekezi maradufu, hivi vinahitaji yambwa zaid ya moja ndo maana iweze kukamilika. Kwa mf. "Mama amemnunulia dada kitabu" ktk mf huu kitenzi ni "amemnunulia" ambapo dada ni yambwa lkn kitenzi bado kinahitaji yambwa nyingine ili ijulikane dada amenunuliwa nini.
Kuna mofu mbalimbali ambazo zinakupa taarifa ya kutambua kwmb hiki ni kitenzi elekezi, au si elekezi hizo tutaziangalia kipindi kijacho mana leo naona mwl. wa psychology yupo mlangoni.