Msaada wenu kwa wanaojua lugha

Msaada wenu kwa wanaojua lugha

mkuu kwanza kitenzi ndio nini!?
na huko yambwa ndio kituo cha kwenda wapi!?
 
Hahahah,Blue Week.
Jamaa kaulizwa na mwanae wa International School sasa anataka jibu,na yeye amekopi anavyojua yeye
 
Haiitwi kitu. mtoa #mada
Kumbuka kuwa sio kila kitu kina majina hapa duniani.
 
Last edited by a moderator:
Kitenzi elekezi/ kitenzi si elekezi
 
Hali ya kitenzi kuhitaji /kutokuhitaji yambwa inaitwaje?

Hali ya kitenzi kuhitaji yambwa inaitwa kitenzi elekezi : kwa mfano, mtoto analilia. Kitenzi ni "analilia" moja kwa moja ni hali ya kitenzi kutoweza kukamilisha taarifa mpk kuwepo na neno au maneno yakukamilisha. Ktk mfano huo inaweza kuwa " mtoto analilia uji".

Hali ya kitenzi kutohitaji yambwa inaitwa kitenzi si elekezi. Kwa mfano " dada anacheka", "kaka analia" "mtoto amelala". ktk mifano hiyo vitenzi ni anacheka, analia, na amelala. Unakutana na vitenzi vya namna hiyo hupati maswali kichwan khs taarifa inayozungumziwa moja kwa moja uanaelewa.

Kwa kuongezea kuna kitu kinaitwa vitenzi elekezi maradufu, hivi vinahitaji yambwa zaid ya moja ndo maana iweze kukamilika. Kwa mf. "Mama amemnunulia dada kitabu" ktk mf huu kitenzi ni "amemnunulia" ambapo dada ni yambwa lkn kitenzi bado kinahitaji yambwa nyingine ili ijulikane dada amenunuliwa nini.

Kuna mofu mbalimbali ambazo zinakupa taarifa ya kutambua kwmb hiki ni kitenzi elekezi, au si elekezi hizo tutaziangalia kipindi kijacho mana leo naona mwl. wa psychology yupo mlangoni.
 
Hali ya kitenzi kuhitaji yambwa inaitwa kitenzi elekezi : kwa mfano, mtoto analilia. Kitenzi ni "analilia" moja kwa moja ni hali ya kitenzi kutoweza kukamilisha taarifa mpk kuwepo na neno au maneno yakukamilisha. Ktk mfano huo inaweza kuwa " mtoto analilia u

Hali ya kitenzi kutohitaji yambwa inaitwa kitenzi si elekezi. Kwa mfano " dada anacheka", "kaka analia" "mtoto amelala". ktk mifano hiyo vitenzi ni anacheka, analia, na amelala. Unakutana na vitenzi vya namna hiyo hupati maswali kichwan khs taarifa inayozungumziwa moja kwa moja uanaelewa.

Kwa kuongezea kuna kitu kinaitwa vitenzi elekezi maradufu, hivi vinahitaji yambwa zaid ya moja ndo maana iweze kukamilika. Kwa mf. "Mama amemnunulia dada kitabu" ktk mf huu kitenzi ni "amemnunulia" ambapo dada ni yambwa lkn kitenzi bado kinahitaji yambwa nyingine ili ijulikane dada amenunuliwa nini.

Kuna mofu mbalimbali ambazo zinakupa taarifa ya kutambua kwmb hiki ni kitenzi elekezi, au si elekezi hizo tutaziangalia kipindi kijacho mana leo naona mwl. wa psychology yupo mlangoni.
Shukran! Nmekuelewa! Ahsante sana mkuu ubalikiwe!
 
Kama mtu hufahamu kitu kwa nini usisome Tu na kupita? Ukichangia kitu nje kabisa na swali nini faida yake? Hapa kila jukwaa lina wataalamu, mtu akiuliza jambo lazima atapata mwanga au majibu ya anachokitafuta. Tubadilike na kwa hakika manufaa ya JF yatabaki palepale. Aksante Sana Rumburia
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom