Msaada wenu ndugu zangu: Ni engine gani inafaa kwenye Toyota Brevis ukiachana na 1JZ & 2JZ

Msaada wenu ndugu zangu: Ni engine gani inafaa kwenye Toyota Brevis ukiachana na 1JZ & 2JZ

Tally q

Member
Joined
Aug 9, 2018
Posts
12
Reaction score
2
Wakuu!

Nina Toyota Brevis ina engine ya 1jz fse D-4. Engine hiyo haipo sawa, mara kwa mara inanisumbua kwa kutoa moshi mwingi na kuzima zima ghafla.

Nimebadili nozzle mkanda mzima, nimebadili sensor zote, enjection n.k bila mafanikio

Baadhi ya mafundi wananishauri nichukue engine nyingine kwakuwa hata nikifanya overhaul katika mashine hiyo baada ya muda mfupi itasumbua tena. Binafsi engine za JZ kwasasa nina wasiwasi nazo.

Hivyo naomba kujuzwa, Ni engine gani tofauti na hizo ambayo itafaa kwenye brevis bila modification yoyote.
 
Tally q,
Duh hii ya leo kali mkuu, labda uipe 2JZ humo japo ni kubwa kuliko 1JZ.

Hizi brevis za bei rahisi ndio madhara yake hayo halafu wanasema zenye mfumo wa D4 au Dual VVT-i haziitajigi mafuta machafu au ya kuokoteza.
 
Hii gari inahitaji matunzo ya Hali ya juu Sana ingawa Kwenye performance iko poa.
 
Weka 1JZ-GTE, 1G- GTE au 1G-GE hizo zitafanya vizuri.

Kama 1G-GE hiyo hata ukiweka mafuta ya kidebe hakuna kusumbua.
 
Weka 1JZ-GTE, 1G- GTE au 1G-GE hizo zitafanya vizuri.

Kama 1G-GE hiyo hata ukiweka mafuta ya kidebe hakuna kusumbua.
GTE hizo bei yake si itakuwa mkasi sana maana sidhani pia kama itakuwa rahisi kupatikana kama hizi za FSE!
 
GTE hizo bei yake si itakuwa mkasi sana maana sidhani pia kama itakuwa rahisi kupatikana kama hizi za FSE!
Kama akiagiza bei ipo juu kiasi, ila hapa Bongo zipo sana atafute kwenye mabaloon, mark/chaser/cresta Gr 80 na Gr 90.

Uganda na Malawi hizo anapata kwenye gari za kuchinjwa.
 
Je ni rafik kwa mazingira ya kibongo bongo maana mafuta yetu sio quality muda mwingine
Hiyo unaweka mafuta ya Kidebe pale Kurasini darajani au kama upo bushi yale ya kuuzwa njiani na unatembea bila kusikia gari ikimiss.
 
Back
Top Bottom