Msaada wenu tafadhari juu ya afya ya mwanangu

Pole. Inaonyesha kwenye kumchoma sindano kuna kosa lilifanyika. Uko sehemu gani? Kama ni Dar kuna hopsital zenye ma-specialist wa watoto au kuna specialist wenye hospital za watoto tu. Mpeleke. Angalia sana kwa sababu hospital nyingi siku hizi hawana utu, hasa hivi vya mtaani.
Changamoto ni kwamba niko nje ya dar. Asante kwa ushauri wako.
 
Habari ndugu zangu wiki kama moja iliyopita mwanangu alilazwa na akachomwa sindano nyingi sana mikononi ni mtoto wa miezi 11.

Sindano zile zilimpelekea kuvimba mkono kwa juu nilivyowauliza hospital wakanijibu hali hiyo itaisha nimesubiri kwa muda wa siku nne sioni dalili za hali hiyo kuisha nikamua kwenda private hospital kupata ushauri.

Nikaambiwa kuwa inabidi apasuliwe mkono maana wanadai kuwa ndani pametengeneza kama jipu.
Nikawajibu acha nirudi kesho.

Kabla sijachukua maamuzi nikaona nitafute Dkt mwingine anipe ushauri pia yeye akaniambia kuwa mtoto kama huyo mishipa yake ni midogo sana kwahiyo kupasuliwa kunaweza kusababisha madhara zaidi akanipa dawa kuwa itamsaidia.

Sasa hapa nimebaki njia panda nimeona nije kwenu hapa maana naamini hapa kuna watu wengi wenye ujuzi na elimu tofauti asanteni.

View attachment 2944366
Pole sana braza.
 
Pole kwa kuuguliwa:
1: Hapo unahitaji utaalamu wa watu wawili: Daktari bingwa wa magonjwa ya watoto pamoja na upasuaji.
A: Kuangalia kama uvimbe umeathiri kwa kiasi gani mfumo wa upitishaji damu kwenda kwenye vidole.(athari ya presha ya uvimbe)

B: Hali ya vidole kwa sasa kama inaruhusu kutibia kwa kutoa DAWA na kuangalia matokeo ya kusinyaa.

C: Kuweka njia ya kupunguza athari ya kuvimba (compartment syndrome).

Unaweza kuwapata hawa kwenye hospitali ngazi ya Wilaya, Mkoa au Rufaa. Au hospital yoyote ya private yenye hadhi sawa au karibu na hizo.
 
Asante sana
 
Dah jamaa wanaweza kukusababishia ulemavu hivihivi

Juzi hapa niliandikiwa sindano nesi mmoja akawa ananitoboa toboa pembeni ya mishipa wakati mishipa inaonekana kabisa kanitoboa sehem nne tofauti kwenye mikono yote miwili na bado kanitoboa pembeni alaf akasukuma dawa kwenye nyama maumivu niliyo yapata kidogo nimuwashe kofi

Inawezekeana dogo dawa ilikua haiingii kwenye mishipa walikua wanasukumia dawa pembeni
 
Kaka na mm hicho ndo kilichotokea kwa mwanangu dawa haikusukumwa kwenye mishipa bali kwenye nyama.
 
Dah hapo wamemsababishia maumivu makali sana na hivyo ni mtoto hasemi siyo poa kabisa yan
 
pole sana mkuu ngoja nimuite baba yangu DR Mambo Jambo
Embu tia neno lolote hapa
Duh kwa kumshauri ampelekea kwa Paediatrician Achunguze Ikibidi Acalculate the risk ya Vitu vyote viwili dawa na Surgery..

Ila kwangu mimi Ningepreffer dawa zaidi, Maana Op inaweza kuongeza tatizo..

Aliwekewa Cannula au?
Ilikaa kwa muda gani?
Walimfunga Plaster kuzunguka mkono?
Maana naona Kama kuna Ka Formation ka Gangrene kanatama kuanza..

Vizuru ni kwamba Hizo ni early signs na Hiyo ni acute Compartment syndrome ambayo imetokana na Poor cannulation kabla haijaanza kupata ublue na uweusi hebu muwaishe hospitali Ya Rufaa ya mkoa Au kanda Sasa hiviiii..

Isaac1
 
Asante sana Dr nina imani ameona hii na atachukua ushauri wako
🙏🙏🙏🙏🙏🙏
 
Pole sana.. ndio matokeo ya kusomea uuguzi vyuo vya ghorofa ya sita
 
Back
Top Bottom