Lovery
JF-Expert Member
- Aug 15, 2014
- 1,555
- 3,208
Habari zenu wakuu,
Naomba nianze moja kwa moja kueleza jambo hili.
Mnamo mwaka 2006 nilikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na binti anaitwa NASRA (si jina halisi) wakati huo alikuwa anafanya kazi za ndani kwa rafiki yake na kaka yangu, wakati huo mimi nilikuwa nikiishi kwa kaka yangu. (R.I.P Bro)
Nilikuwa sina dira ya maisha wakati huo nikawa najiendekeza na mafunzo ya computer,
Badaa ya mahusiano ya muda kama miezi 6, binti huyo akawa ameondoka yani kaacha kazi na sikuwa na simu kujua kaelekea wapi kwani wakati anaondoka nilikuwa safari kwa wazazi wangu.
Baada ya miezi kadhaa nikapata taarifa zisizo rasmi ya kwamba kaolewa kijiji fulani ila kajifungua mtoto kafanana na mimi sana, kwakuwa alikuwa kaolewa nikaona ni taarifa za uongo hata hivyo wote hatukuwa na simu.
Leo kanitafuta baada ya miaka 10 kupita na anadai yule ni mtoto wangu ila alimpatia mtu kwakuwa maisha ndio yalimfanya afanye hivyo kwasababu mimi nilikuwa bado hata sabuni naomba, japo mtoto anahudumiwa na yule jamaa na mwanamke ana ajira nzuri baada ya kusoma tena.
hivyo ananiambia niende kumuona mtoto na tuzungumze jambo la kufanya ili anipatie mtoto wangu.
Najiuliza je nianzie wapi endapo ikiwa kweli mtoto ni wangu?
Mtoto anatumia jina la baba mwingine kisheria inakaaje?
Familia ya yule bwana wataniona mtu wa aina gani?
HAKIKA SIJUI PAKUANZIA NAOMBENI MSAADA WA USHAURI.