Msaada wenu wa mawazo ni muhimu sana kwangu

Msaada wenu wa mawazo ni muhimu sana kwangu

Huyu bwana aliyepewa mtoto hakubahatika kumuoa huyu mwanamke maana walikuwa wapenzi tu, ila aliolewa na mtu mwingine kabisa na yeye akabakia kama mzazi mwenzake, japo huko pia akawa kaachika na sasa anaishi peke yake.
Kizungumkuti kwakweli.
Usikubali kufanya mazungumzo yoyote bila kuwa na uhakika kama mtoto ni wako.
DNA ihusike ndio mengine yafuate.
 
Pole,ushauri wangu ni huu,achana na kila kitu Fanya yako,mtoto akiwa mtu mzima atakutafuta Kwa muda wake,huu mtihani una vipingamizi na jamii haitakuchukulia vizuri.
 
Pole sana kwa hyo baada ya kuachika ndio anakutafuta siyo?? Asingeachika inaonekana asingekua na mipango nawe,ila sbu ka kwama anatafuta hisani.. Bas sawa ni hiv bro..kwanza huna hakika km kwel mtoto ni wako ila kama ni wako mwambie tu amweleze mwanao ukwel na mtoto bila kumlazimisha aamue yeye mwenyewe. Sawa kama ni mwanao kwel hata dunia ikiisha leo hii bado atabaki wako tu haitabadilika kamwe,lakin mtoto anapokeaje haya? Unajua angekua chin ya miaka 5 na ukawa nae karib sana ana sahau yte ya zaman bt kashafikisha ten years unadhan kumbukumbu zitafutika?

Mwsho ni kwamba mwambie hyo mwanamke amwambie kwanza ukwel,then wewe uanze kujenga mazoea kdgo kdgo hata miaka mitatu au minne then ule upendo utamwngia mtoto polepole na mwsho atajivunia kua wewe unampenda.

NB: SIKUSHAURI HATA KIDGO KUISHI NA HUYO MWANAMKE.
Asante sana mkuu kwa mchango wako, bila shaka haya uliyonishauri ndio nitaanza nayo kwanza
 
Kizungumkuti kwakweli.
Usikubali kufanya mazungumzo yoyote bila kuwa na uhakika kama mtoto ni wako.
DNA ihusike ndio mengine yafuate.
Asante sana mkuu maana nimekuwa njia panda
 
Nasikiaga ni ghali siyo chini ya laki moja kwa hospital sijajua,
Kwakuwa ni jambo muhimu sana nitafanya hivyo kwasababu naweza kukwepa ikawa kweli ni damu yangu na baadae nitaonekana nimekosa utu.
 
Kwakuwa ni jambo muhimu sana nitafanya hivyo kwasababu naweza kukwepa ikawa kweli ni damu yangu na baadae nitaonekana nimekosa utu.
Nikweli Fanya hivyo mkuu, kwasababu wewe huna kosa coz ulikuwa hujui km wskati wa mahusiano yenu alipata mimba, tena ikiwezekana km ikijulikana mtt ni wako na mama mtu hajaolewa, mnaweza Ku up date penzi lenu mkaoana mkamlea mmt
 
Habari zenu wakuu,

Naomba nianze moja kwa moja kueleza jambo hili.

Mnamo mwaka 2006 nilikuwa katika mahusiano ya kimapenzi na binti anaitwa NASRA (si jina halisi) wakati huo alikuwa anafanya kazi za ndani kwa rafiki yake na kaka yangu, wakati huo mimi nilikuwa nikiishi kwa kaka yangu. (R.I.P Bro)

Nilikuwa sina dira ya maisha wakati huo nikawa najiendekeza na mafunzo ya computer,

Badaa ya mahusiano ya muda kama miezi 6, binti huyo akawa ameondoka yani kaacha kazi na sikuwa na simu kujua kaelekea wapi kwani wakati anaondoka nilikuwa safari kwa wazazi wangu.

Baada ya miezi kadhaa nikapata taarifa zisizo rasmi ya kwamba kaolewa kijiji fulani ila kajifungua mtoto kafanana na mimi sana, kwakuwa alikuwa kaolewa nikaona ni taarifa za uongo hata hivyo wote hatukuwa na simu.

Leo kanitafuta baada ya miaka 10 kupita na anadai yule ni mtoto wangu ila alimpatia mtu kwakuwa maisha ndio yalimfanya afanye hivyo kwasababu mimi nilikuwa bado hata sabuni naomba, japo mtoto anahudumiwa na yule jamaa na mwanamke ana ajira nzuri baada ya kusoma tena.

hivyo ananiambia niende kumuona mtoto na tuzungumze jambo la kufanya ili anipatie mtoto wangu.

Najiuliza je nianzie wapi endapo ikiwa kweli mtoto ni wangu?
Mtoto anatumia jina la baba mwingine kisheria inakaaje?
Familia ya yule bwana wataniona mtu wa aina gani?

HAKIKA SIJUI PAKUANZIA NAOMBENI MSAADA WA USHAURI.
Pole sana p
 
Back
Top Bottom